December 29, 2018


Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nswanzurimo amesema wapo tayari kwa ajili ya kupambana na kikosi cha Yanga ambacho mpaka sasa bado hakijapoteza hata mchezo mmoja katika Ligi baada ya kucheza michezo 17.

 Nswanzurimo amesema kuwa rekodi zote duniani zimewekwa ili zivunjwe na hilo linawezekana kwenye mpira kutokana na mbinu alizowapa wachezaji wake kuweza kufanikiwa kuitibua rekodi ya wapinzani wao.

"Tunawatambua wapinzani wetu wapo vizuri, ila haitupi mashaka kuweza kupambana nao huu ni mpira tutaonyesha uwezo wetu na tutacheza tukiwa ni timu mpaka kufanikiwa kupata ushindi ambao tunatarajia.

"Wao wanatafuta pointi tatu nasi tunahitaji pia pointi tatu, hivyo ushindani lazima utakuwa mgumu na nimewaambia wachezaji wajitume na wajiamini kila kitu kinawezekana kwa kuwa hakuna mwenye uhakika wa kushinda kama hatajituma," alisema Nswanzurimo.

Mbeya City wamecheza michezo 17 ya Ligi wakiwa nafasi ya 7 baada ya kukusanya pointi 23 watakutana na vigogo Yanga ambao wana pointi 47 wakiwa ni vinara wa Ligi kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic