YANGA WAICHEZEA LULU
Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa Yanga wameichezea lulu.
Bwire amesema Yanga wameichezea ni kutokana na mchezaji Emmanuel Martin aliyeko kwa mkopo kuibuka shujaa kwa kufunga bao hilo.
Martin ambaye yuko Ruvu kwa mkopo alifunga bao hilo pekee na kuwafanya Ruvu Shooting kuibuka wababe kwa kubeba pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Mlandizi, Pwani.
"Lulu waliyoiacha imekuwa na thamani kwetu, waliichezea na hawakuipa nafasi lakini kwetu imeleta matunda kwa kufunga goli ambalo limetupa alama tatu leo"
Licha ya Bishara kufungwa, Bwire amewasifia vijana hao kuwa wamecheza soka la zuri na la kuvutia zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment