December 28, 2018







KUNDI A
Waydad 
Sundowns
Asec Mimosa
Lobi Star


KUNDI B
Esperance
Horoya
Orlando Pirates
FC Platnums


KUNDI C
TP Mazembe
Ismaily
Constantine
Club African

KUNDI D
Al Ahly 
Simba
JS Soura
AS Vita

3 COMMENTS:

  1. Safi sana, Asante sana Mnyama kwa kutuwakilisha vyema Africa. Sasa wakati umefika wa kulisahau neno kuwakilisha ni wakati wa kutanguliza mbele neno kupambana. Wakati wa vita umefika na jeshi legelege ndilo la kwanza kuangamia. Tena na tena Simba warekebishe beki yao waache kutojali maoni ya wadau mbali mbali nchini na wa nchi jirani kama vile kocha wa Nkana FC kuwa Simba wa hivyo kwenye baki yao na wasipojirekebisha basi itakuwa moja ya timu ya hivyo kwenye hatua ya makundi. Binafsi ningewaomba Simba waachane na suala la kutafuta fowadi na badala yake watafute beki kisiki mahiri wa kati kama wameshindwa kumuamini Juuko Murshidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli beki wa kati mwenye kasi anahitajika lkn pia bado foward mwenye speed na upambanaji wa aina ya Kagere anahitajika sana.Kwa mtazamo wangu hakuna kundi rahisi na timu zote zitapambana kutafuta kitita cha mabilioni hivyo timu yetu SIMBA ilijue hilo na wajitambue kuwa mapambano hayo si narenare.

      Delete
  2. Al Ahly inasemekana imefanya na inaendelea kufanya usajili wa kufa mtu ikiwemo pamoja na kuchukua mchezaji kutoka ligi ya Uingereza na wachezaji kadhaa mahiri kutoka ndani ya Egypt na nchi kama Angola na kadhika ili kujiimarisha kuulekea michezo ya hatua ya makundi. Kwa hivyo mshindi wa pili wa kombe hilo la klabu bingwa Africa anahaha kujiimarisha lakini bado hatujaona jitihada zozote za maana zinazochukuliwa kwa upande wa Simba kukiimarisha kile kikosi licha ya mapungufu kadhaa yanayoonekana wazi kwenye kikosi chao.Utashangaa kusikia viongozi wa Simba wakisema eti wanasubiri ratiba itoke ndio waanze kuzungumza na kocha wao kuhusiana na kikosi chao? Simba kama kuna uzembe wa aina fulani unaendelea kwenye timu yao hivi sasa labda hapo awali viongozi ilikuwa ni kiki za uchaguzi basi na sasa hivi inaonekana wamerelax. Hakika Mo hawezi kufanya kila kitu peke yake. Mwaka jana alifanya ujasiri wa mapinduzi makubwa kama mabadiliko ya makocha nakadhalika lakini cha kushangaza inaonekana kama Mo hana uungwaji mkono wa nguvu moja kiutendaj na baadhi ya viongozi wa Simba na hata simba kufungwa na Mashujaa ni dalili yakwamba uchaguzi uliopita pale klabuni kuna walakini miongoni mwa watendaji wake. Akina Salimu Try again kwa kushirikiana na Mo waliiongoza Simba vizuri na ni mapema mno kuanza kuuhukumu uongozi mpya kutokana na kasoro zinazojitokeza lakini kuna mambo yanaanza kwenda hovyo ndani ya Simba. Mfano hata Kapombe kabla hajaumia kocha wa Simba alikuwa akiomba kutafutiwa mbadala wake lakini suala hilo lilichukua muda kutekelezwa. Sula la beki wa kati na kiungo cha chini cha uhakika mbadala wa Mkude kama atapata majeraha, pamoja na kutafutwa uongezo wa fowadi mmoja wa nguvu kuongezea nguvu fowadi ya sasa ni suala la lililojadiliwa kwa muda mrefu na wadau mabali mbali kuwa ni muhimu kutokana na uzito wa timu hatua ya makundi lakini utaona hakuna kilichofanyika na kwa kiasi fulani is too late. Kujidanganya kuwa timu uliopo Simba inatosha kwenda kupambana hatua ya makundi na kutoa matokeo chanya sidhani kama timu hiyo wanayo. Wachezaji wanao lakini sio wale wenye moyo wa kupambana wengi wao ni magoigoi.Mtizame Mohamed Husein goli la Bwalya alivyokuwa akimsherehesha Chisala wa Nkana kama vile yupo kwenye mazoezi. Si bora angekwenda kumvamia yule mchezaji na kupata kadi kuliko kuruhusu goli. Kazi kubwa ya beki wa pembeni ni kumzuia winga asipige krosi kwani krosi mara nyingi huwa ina madhara pengine kuliko penalt hata magoli mawili ya Simba dhidi ya Nkana ni matokeo ya krosi. Tungewaomba viongozi wa Simba waamke aidha kwa kuwaweka chini baadhi ya wachazaji wao kujua nini kinaendelea kwani hawapo pale simba kuuza uzuri wapo kazini na wawe wepesi wa kujifunza kutoka kwa wenzao kwani Chama amekuja juzi tu lakini angalia anavyo haha uwanjani mpaka dakika ya mwisho. Utasikia tatizo lao kubwa ni kukata pumzi kila dakika zikisonga mbele sasa kuna haja gani kuwa na wachezaji wa wavivu? Hivyo mchezaji professional analipwa kwa ajili ya kucheza mpira anashindwa kujitengenezea pumzi zake binafsi kuwa za kiushindani kutokana na level yake ya mchezo? Mchezaji gani anaesubiri kutafutiwa pumzi na kocha? Mazoezi ya kukimbia ni mazoezi mama ya pumzi na kwa kiasi fulani ni maamuzi ya mtu au mchezaji binafsi na wala hayana gharama ya muda au fedha ni akili ya mtu basi. Kwa upande mwengine kweli usajili ni gharama lakini vipi Simba ishindwe hata na Yanga kutafuta wachezaji kwa wakati.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic