December 3, 2018


Kikosi cha Tanzania Prisons chenye maskani yake mkoani Mbeya kimepania kupata pointi tatu mbele ya Yangaa ambayo bado haijapoteza mchezo mpaka sasa ili waweze kujinasua kutoka nafasi ya 19 waliyopo kwa sasa.


Prisons FC, haijawa na matokeo mazuri msimu huu kwa kuwa katika michezo 14 waliyocheza wameshinda mchezo 1 tu na kupoteza michezo 6 huku wakiwa na sare 7 ambazo zinawafanya wawe na pointi 10.


Beki  tegemeo wa Prisons, Salum Kimenya amesema wamejipanga kuhakikisha wanapindua meza kibabe kwa timu watakazokutana nazo.

"Tunajua tupo katika nafasi mbaya ambayo haitufarahishi wachezaji na viongozi hivyo tunatakiwa kushinda mchezo wetu wa leo dhidi ya Yanga ili tujinasue katika nafasi tuliyopo.


"Ushindani ni mkubwa nasi tumejiandaa kuweza kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani, tunaamini utakuwa ni mchezo mgumu ila tunatambua tukipata matokeo tutatoka hapa chini tulipo," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Hayo ni maneno tu ila ki ukweli timu hizi ndogo mipango na ubora wa kuzifunga timu kama Yanga, Simba na Azam hawana, hata wakishinda inakuwa kama bahati sio kwa kuwa wana kiwango cha kivileee.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic