May 19, 2017

PICHA ILIYOZAGAA IKIONYESHA MMOJA WA MADEREVA AKIONYESHA WALIVYOSHAMBULIWA KWA RISASI HUKO DR CONGO NA WENZAO KUTEKWA.


Kuna taarifa tumepokea kuwa madereva kadhaa ambao wanaendesha magari yanayomilikiwa na Zacharia Hans Poppe, wametekwa nchini DR Congo.

Taarifa zilizotufikia kuwa ni madereva zaidi ya wanne wametekwa na watu wanaoaminika ni watekaji katika moja ya misitu nchini humo.

Kabla ya utekaji huo, imeelezwa watekaji hao walitumia risasi za moto kuwashambulia madereva hao.  Bado tunafuatilia kujua ilikuwaje.


Bado tunafanya juhudi za kumpata Hans Poppe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba atueleze.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV