December 28, 2018


IKIWA leo droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19 inatarajiwa kupangwa, Simba ni miongoni mwa timu ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nahodha na mshambuliaji wa Simba, John Bocco amefunguka kwamba hawaogopi kupangwa na klabu yoyote ile.

Simba walifanikiwa kutinga hatua ya makundi Afrika baada ya kuitoa Nkana ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3 ushindi wa jumla baada ya kufungwa mabao 2-1 ugenini na kushinda 3-1 nyumbani.

Bocco amesema kwamba baada ya kutinga hatua hiyo watajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri hata kama ikitokea watapangwa na timu ambazo zinaonekana kuwa juu kuliko wao.

“Tumepambana kwa ushirikino mzuri na kufanikiwa kufikia lengo letu la kwanza kufika hatua ya makundi ni jambo jema kwetu na tunatambua kwamba tuna kazi ngumu mbele.

“Kuhusiana na timu hizo kama TP Mazembe na wengineo, naamini tutaenda kujipanga kutokana na timu ambazo tutakutana nazo, tuna kocha mzuri tuna benchi zuri na lina uzoefu na michuano hii pia wachezaji wenye uzoefu na michuano hii hivyo naamini kwamba tutafanya vizuri,” alisema Bocco.

Nje ya Simba timu nyingine zilizofuzu hatua ya makundi ya kombe hilo ni Esperance ambao ni mabingwa, TP Mazembe, Orlando Pirates, Mamelodi Sundowns, CS Constantine, FC Platinum, Ismaily SC na Lobi Stars.

Zingine ni Wydad Casablanca, AS Vita, JS Saouara, Asec Mimosas, Horoya AC na Club Africain, Al- Alhly.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic