SIMBA WATOA TAMKO KUHUSIANA NA OKWI KWENDA KAIZER CHIEFS
Na George Mganga
Uongozi wa Simba umepiga chini ofa ya klabu kutoka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs inayomhitaji mshambuliaji wake, Mganda Emmanuel Okwi.
Taarifa kutoka Simba zinaeleza Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbegiji, Patrick Aussems ameikataa kwa kuwa anamtegemea Okwi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Imeelezwa kuwa Kaizer wamevutiwa na Okwi ambaye alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita na ikitajwa wametangaza dau la USD 30,000 za kimarekani.
Licha ya kuweka ofa hiyo mezani, Aussems amekataa kukubaliana nayo na badala yake akiwataka mabosi wake wahakikishe Okwi haondoki Msimbazi.
Simba hivi sasa inajiandaa kuja kukabiliana na Nkana Red Devils katika hatua ya kwanza ya CAF Champions League katika mchezo utakaopigwa huko Zambia Disemba 14 2018.
Hivi ni USD 30 kweli? Hii blog inaongoza kwa Makosa ya kiuandishi!
ReplyDeleteAisee naipenda hii blog ila ubabaishaji wa namna hii na uandishi wa kizwazwa unanikatisha tamaa sana!! usd 30 kweliiiiii?????
DeleteWatanzania jinsi tusivyojitambua huyo tuliyemuita muhenga anagombaniwa Africa kusini kwa dau la kufuru. Yaani mtu ukiwa na malengo yako fanya lakini usije ukajindua kusikiliza wabongo wanasema nini. Kuna hata baadhi ya wanaojifanya waandishi wa michezo nchini walimkalia kooni Okwii.Aaa eti sijui mzee. Aaa eti miaka ya kudanganya. Eti sijui msimu huu hawezi kungara tena umri umekwenda. Yaani uchawi mtupu kama vile hawana kazi za kufanya.Watanzania kwa majungu yasio na msingi kwetu sisi ndio big deal lakini vya kutunufaisha hatuna habari navyo. Kuna wachezaji wazuri tu tumewastaafisha kucheza mpira wangali bado wanauwezo kutokana na majungu yetu yaani ujinga mtupu .Nadhani kama Okwi angekuwa mbongo basi tena ila waganda wanajitambua na ndio maana mara nyingi kila tunapokutana nao wanatuchapa. Ukienda pale Egypt basi utawakuta wachezji wana miaka mpaka arubaini na ushee 40 na bado wapo kwenye fomu na husikii kutokezea mgonjwa wa akili akamwita mchezaji mzee kwao wao thamani ya mchezaji kiheshima huwa inazidi zaidi mpaka yeye mwenyewe aamue kustaafu. Watanzania lazima tubadilike la sivyo hatutafika kokote. Na ndio maana akina Okwi, Kagere, Chama,hata Juko,Simba inabidi ifanye kazi ya ziada kuwazibiti wasiondoke kutokana na kutakuwa nje wakati vijana wetu hata mmoja hakuna alieivutia timu yeyote ya maana mpaka hivi sasa.Simba wana benchi la ufundi lililoshiba mchezaji mwenye kujitambua lazima kiwango kitapanda na ndio maana kila siku zikienda mbele pale Simba wachezji wa kigeni wanazidi kuonekana lulu ni vizuri kuwashauri vijana wetu kuongeza ari ya ushindani nao waonekane kuliko kupika majungu yasio na maana kwani hayatatusaidia kitu.
ReplyDeleteBe serious bwana USD 30 tens
ReplyDeleteKwa figure aliyoiweka ni wastani Milioni 66 za kibongo, Okwi wa kwenda kwa dau dogo la namna hiyo! Hawa jamaa watufafanulie zaidi. Hilo ni dau la Kumnunua KINDOKI bhana sio OKWI!.
ReplyDeleteUSD30000 nyie vp amjui kuxoma nn it means 30000×2000+
ReplyDelete