December 8, 2018


Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania Bara kupitia (TPLB) imefanya mabadiliko ya michezo mitatu ya ligi.

Ratiba hiyo inaonesha mchezo namba 159 kati ya Yanga SC na Biashara United ambao utachezwa kesho December 09 katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, umesogezwa mbele kwa masaa matatu kutoka saa 10:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku.

Pia, mchezo wa kiporo wa Simba dhidi ya KMC umepangiwa tarehe na sasa utachezwa Jumatano ya Disemba 19 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam majira ya saa 12:00 jioni.

Mbali na mchezo huo, mchezo namba 170 kati ya KMC na TZ Prisons uliokuwa uchezwe Disemba 17 umerudishwa nyuma na sasa utachezwa Disemba 15 katika dimba la Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic