December 28, 2018



UONGOZI wa Singida United umesema unatambua upana wa kikosi cha Simba hali iliyowafanya waingie mafichoni kujipanga kabla ya kuibukia Taifa kuchukua pointi tatu.

Singida United watamenyana na Simba kesho katika uwanja wa Taifa, kwa sasa wapo Dar es Salaam wakiwa wanajipanga kuwatungua wapinzani wao.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wamejipanga kurejea na ushindi nyumbani bila kujali aina ya timu watakayokutana nayo.

"Kikosi kimewasili Dar na tuweka kambi mafichoni kikiwa na wachezaji wote muhimu kwa kazi moja tu pointi tatu ili kujiweka sawa katika msimamo wa ligi kuu bara ila angalizo kwa simba kuwa tumejipanga vizuri sana.

"Tunawaheshimu wapinzani wasitegeme mteremko, kocha Suleiman Jabir akisaidiwa na Shadrack Nsajigwa 'fusso' wamefanya kazi yao kuweka ubora wa kikosi," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic