Cyril Patrick Munish mshindi wa droo ya 48 kwenye promosheni ya Shinda zaidi na SportPesa amejikomboa na kumiliki mtaji huku akielezea mikakati yake Kabambe baada ya ushindi huu.
Huyu ni mkazi wa Shinyanga na timu ya ushindi imemfuata mpaka nyumbani kwa kwake na kumkabidhi Bajaj Re.
Akizungumza na Sportpesa mara baada ya kukabidhiwa chombo chake Munishi Alisema alianza kucheza na SportPesa baada ya kuona washindi wengine wakitangazwa kwenye vyombo vya habari.
"Mimi nilianza kucheza na SportPesa ikiwa ni muda mchache tangu nimeanza kufuatilia kwenye televisheni nilipoona wengine wanashinda niliamini hata mimi naweza kucheza na kushinda na kile nilichokuwa naomba naona sasa kimetimia" alisema Munishi.
Aidha, mshindi huyo aliweka wazi mikakati yake baada ya kukabidhiwa bajaj "kama nilivyowaeleza Mimi ni mfanya biashara nauza dagaa huko nyuma nilikuwa naweza chukua gunia moja na kuingiza sokoni lakini hivi sasa ntaboresha zaidi badala ya gunia moja ntachukua magunia zaidi maana kipato kitaongezeka "
Hata Hivyo mbali ya Suala la biashara anaamini bajaj hiyo itamwezesha kupambana na kumiliki nyumba yake binafsi pamoja na kumsaidia kwenye mahitaji ya kila siku.
Munishi aliwaomba watanzania kuichangamkia fursa hii kutoka SportPesa na kuwataka kuachana na fikra mgando huku akidai kuwa kucheza mara nyingi ndio kujiongezea nafasi ya ushindi.
Mbali ya kushinda bajaj SportPesa inakukumbusha kucheza jackpot ambayo imesimamia kwenye zaidi ya sh. Milioni 429 hii inampa mtu nafasi ya kubashiri Mechi 13 na akifanikiwa kuzibashiri mechi zote kwa usahihi ataondoka nazo zote lakini yule anayefanikiwa kubashiri Mechi 10, 11, na 12 kwa ufasaha anaondoka na bonus ambayo ni ya utofauti na wala haigawanyiki.
Wiki hii SportPesa imepata mshindi wa bonasi ya Jackpot mara baada ya kubashiri mechi 12 kwa usahihi na kujishindia kiasi cha shilingi milioni 32,115,560.
Katika msimu huu wa sikukuu wateja wa mitandao yote ya simu wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka SportPesa kama Bajaji, Jezi za Simba na Yanga, Smartphone (simu janja) pamoja na safari ya kwenda kushuhudia ligi kubwa mbili suniani yaani Hispania na Uingereza.
0 COMMENTS:
Post a Comment