Kikosi cha Singida United ambacho msimu huu bado hakijarejea kwenye ubora wake kimetamba kuyatumia mashindano ya kombe la Shirikisho kuwa sehemu ya maandalizi ya kuiwinda Simba.
Singida United watacheza na Simba Jumamosi katika uwanja wa Taifa, ratiba yao ilirudishwa nyuma na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na uwanja kuwa na matumizi mengine.
Ofisa habari wa Singida United, Cales Katemana amesema watatumia mashindano ya Shirikisho kuandaa kikosi kitakachoisimamisha Simba uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu.
"Tuna kikosi imara na makini ambacho kimeanza kuonyesha maajabu kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambapo tumefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 Arusha United.
"Ni muda wetu kutumia fursa ya mashindano haya kuwaandaa wachezaji wetu kuelekea katika mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, tunajua haitakuwa rahisi ila tunahitaji pointi tatu," alisema Katemana.
Singida United wana pointi 19 wakiwa wamecheza michezo 16 na wameshinda michezo 5 sare 4 na wamepoteza michezo 7 wakiwa nafasi ya 12.
0 COMMENTS:
Post a Comment