Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Tukuyu Star watakaovaana nao leo kwenye kombe la shirikisho.
Abdul amesema kwamba kilichobaki kwa sasa ni kumaliza mchezo uwanjani kwani kazi ya mwalimu imekamilika hasa baada ya kufanya maandalizi kwa muda mrefu.
"Hesabu zetu ni kupata matokeo na morali ni kubwa kwetu hivyo tuna imani ya kuibuka na ushindi, mashabiki watupe sapoti na dua zao ni muhimu kwetu.
"Maandalizi kwa wachezaji yamekamilika ukizingatia tulianza kujiaandaa mapema baada hivyo tuna nafasi ya kupata matokeo yatakayotusaidia kusonga mbele," alisema.
Mashindano ya kombe la Shirikisho yanaendelea kwa sasa ikiwa ni msimu wa nne ambapo bingwa wa kwanza alikuwa ni Yanga kisha akafuata Simba na anayeshikilia kombe kwa sasa ni Mtibwa Sugar ambaye juzi alitolewa katika mashindano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment