December 30, 2018


BAADA ya Droo ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kupangwa na Simba kuwapangiwa kundi D, mchezaji wa zamani wa Simba na Kocha wa Lipuli, Seleman Matola amewapa tahadhari wachezaji na viongozi wa Simba.

Matola alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba waliofanikiwa kutinga hatua ya makundi mara ya mwisho mwaka 2003 baada ya kuitoa Zamalek ya Misri kwa penati 4-3.

Matola amesema kwa hatua ambayo Simba wamefika pamoja na aina ya kundi walilopangiwa wanapaswa waongeze umakini na kupambana kufa na kupona.

"Wachezaji wasifikirie kila kitu ni rahisi wakabweteka kwa hatua ambayo wamefika watakuwa wanajidanganya kwani hatua ya makundi ni ngumu endapo watakuwa hawana morali ya kupambana na kucheza wakiwa ni timu," alisema.

Timu ambazo zipo kundi D ni pamoja na JS Saoura ya Algeria, As Vita ya Congo na Al- Alhly ya Misri ambapo mechi ya kwanza Simba wataanza nyumbani kucheza na JS Saoura Januari 11.

2 COMMENTS:

  1. USHAURI WA MATOLA NI MZURI. TATIZO HAKUNA KIONGOZI WA KULIFANYIA KAZI. TUKITOA USHAURI TIMU IKAZE TUNATAKA MAGOLI, YUPO KIONGOZI ANAKUJIBU OOH MPIRA WA MIGUU SIO NETIBOLI. SASA HAMASA UNAFANYAJE BILA KUHIMIZA USHINDI MKUBWA? VIONGOZI BADILIKENI MUHIMIZE TIMU ICHEZE KUTAKA MAGOLI. MPIRA NI MAGOLI. USHINDI NI MAGOLI. KAULI MBINU YANGU MIMI INGEKUWA '' LAZIMA TUSHINDE TUNATAKA MAGOLI''

    ReplyDelete
  2. Matola amaetoa ushauri mzuri kwani suala la umakini ndio tatizo la timu au wachezaji wa kitanzania kufungwa magoli ya kizembe au kupoteza nafasi za wazi za kufunga kizembe. Lakini kuna watanzania bado wana mawazo mgando, mawazo au ushauri wa hovyo kuhusiana na ushiriki wa Simba kwenye hatua hii ya makundi.Mfano Shaffih Dauda,nadhani labda anasukumwa na chuki zake binafsi juu ya Simba hakupendezewa kuona Simba imeingia kwenye hatua ya makundi. Nakumbuka hata Simba ilipopoteza kule kitwe Zambia kwa Nkana alichamba sana na kuipeleka Nakana katika hatua ya makundi kabla hata mechi ya marudiano Daresalam. Sasa kaja na ushauri wa kuishauri Simba kwamba katika ushiriki wao huu wasiende na matarajio yeyote ya kushinda timu yeyote kwakuwa Simba ni timu nyonge kuliko zote na kama vile haitoshi akisisitiza kuwa hata ukanda anaotoka Simba ni ukanda mnyonge kwa hivyo hawana chochote cha maana Simba watakachokwenda kufanya mbele ya wapinzani wake. Kwa kweli mimi nilikuwa namuwekea heshima fulani hivi Shaffih Dauda kwa kuona katembea kidogo labda atakuwa si Mpumbavu lakini baada ya kuona hizi clip za kuishuri Simba ikubali kuwa nyonge kwenye group lao nilitamani kama kungekuwa na namba maalum ya simu ya vyombo vya dola kuripoti wasaliti wanaopita mitaani kueneza hali ya kutokujiamini kwa vijana wa kitanzania. Shaffih Daudi ni Coward na hafai kwenye jamii yetu ya sasa ya Tanzania. Yeye kama kaona Simba haiwezi basi angawashauri akina kichuya wapambane angalau waonekane waje kuwa msaada kwa timu ya Taifa lakini Shaffih Dauda kwa maoni yake tayari ameshazigawa point zote za Simba kwa wapinzani wake. Kwani Ulimwengu na Shaffih Dauda nani ana ufahamu mzuri wa mashindano hayo? Thomas Ulimwengu anasema mazali Simba wameingia hatua ya makundi lazima watakuwa wazuri. Miaka miwili nyuma iliyopita Tanzania ilikuwa haina commercial plane hata moja, yaani Tz ilikuwa haina ndege hata moja ya kibiashara lakini leo hii Tanzania inamiliki among the beautiful planes in the planet zenye uwezo kutoka Tanzania hadi China kama kwenda moro . Mabadiliko kuelekea kwenye Tanzania ya ushindani yanaendelea kwa kiasi ya ajabu kwenye taasisi mabali mbali na asiayaamini muache abakie huko ila ni bora afumbe mdomo wake kuliko kuwakatisha tamaa wengine tena kupitia vyombo vya habari huko ni kuunajisi uwana habari. Ukizungumzia ranks kuwa level yake Simba si ya kwenda kushindana na akina Al Ahly vipi kama Khassani Mwakinyo angemshauri mtu kama Shaffih Dauda baada ya kupata mwaliko yakwamba anakwenda kupigana na bondia bora wa Uingereza, bondia namba nane bora duniani kwenye uzito wa kati wakati Mwakinyo hata hiyo rank ilikuwa itafutwe kwa tochi . Nini Shaffih Dauda angemshauri mwakinyo? Labda angemshauri Mwakinyo aachane na ngumi. Watanzania lazima tuweke utanzania wetu mbele tuwache ubinafsi Simba inaliwakilisha Taifa kama inakukera ni bora kaa kimya. Simba uwezo wa kashiriki kwa mafanikio mashindano haya anao mkubwa hakuna shaka hata kidogo wito wangu hasa kwa wachezaji wazawa ndani ya Simba wao ndio wanaotakiwa kujiandaa kwa jihadi kwa kila mechi watakayopata nafasi ya kucheza. Wanatakiwa kustep up kuibeba Simba akina Kagere ni ziada tu kwani kujitoa kwenu kutazidi kuwaongezea morali wachezaji wageni.Vile vile kujitoa kwenu ni moja ya njia ya kujitangaza ili kupata nafasi ya kusonga mbele zaidi ni mashindano makubwa ya kwenda kutengeneza C.V yako kama kweli una nia ya kwenda kucheza nje ya tanzania kwa maslahi mapana zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic