December 3, 2018


Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, anapigiwa upatu kuhamia klabu ya Inter Milan msimu huu wa joto. (Sun)

Ozil, ambaye aliachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Bournemouth wiki iliyopita alikosa derby ya London kaskazini kutokana na maumivu ya misuli, ilisema Arsenal. (Daily Mail)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri ya kwamba hakuwa na uhakika ikiwa Ozil angelihudhuria mechi ya Arsenal dhidi yaTottenham ambapo waliibuka kidedea. (Independent)

Aston Villa imefanya mazungumza na Chelsea kuhusiana na uhamisho wa Tammy Abraham kwa mkopo - wana matumaini makubaliano hayo ya msimu mzima na shambuliaji huyo wa miaka 21 hayatatibuka. (Birmingham Mail)

Kumekuwa na tetesi kuwa kiungo wa kati wa Napoli Piotr Zielinski, 24, huenda analengwa na Liverpool, klabu hiyo imeripotiwa kuwa na mpango wa kutia saini makataba mpya katika klabu hiyo ya Italia. (Calciomercato)

Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amezua zogo lingine kwa kumshambulia kwa maneno makali Paul Pogba.

Inadaiwa kuwa Mourinho alisema mchezaji huyo wa Ufaransa ni "kirusi" kufuatia sare ya mabao mawili kwa mawali kati ya klabu hiyo na Southampton siku ya jumamosi. (Daily Record)

Mkuu wa Everton Marco Silva anasisitiza kuwa meneja mwenzake Jurgen Klopp hakuomba msamaha kwa kukimbilia uwanjani wakati alipokuwa anashangilia ushindi wa dakika za mwisho mwisho wa Liverpool dhidi ya Merseyside. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Manchester United Fred, 25, ambaye amecheza mechi sita pekee katika ligi ya primia msimu huu amekwazika na ukosefu wake kushirikishwa kati timu.

Hali hiyo pia ilimfanya kuachwa nje kikosi kilichocheza hivi karibuni na Brazil. (Manchester Evening News)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasisitiza kuwa mlinzi wa Juan Foyth mwenye umri wa miaka 20 ni mmoja wa wachezaji wake waliyoonesha umahiri mkubwa katika mechi kati yao na Arsenal, licha ya kosa alilofanya ambalo lilipelekea wao kushindwa kayika uga wa Emirates. (Football.London)

Kiungo wa Arsenal Lucas Torreira amedokeza kuwa ushauri wa Unai Emery wakati wa mapumziko ilichangia ushindi wa Tottenham katika Derby ya North London. (ESPN)

Shabiki wa Tottenham alikamatwa siku wa Jumapili kwa kosa la kutupa ganda la ndizi uwanjani baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kuifungia Arsenal bao dhidi ya klabu hiyo. (Daily Telegraph)

Kwa mujibu wa BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic