YANGA WANENA JAMBO KUHUSIANA NA MECHI YA LEO DHIDI YA TUKUYU STARS
Uongozi wa Yanga umesema kuwa hauna mashaka na kikosi cha Tukuyu Stars ambacho watacheza nacho katika mchezo wao wa leo wa Kombe la Shirikisho.
Yanga ina kumbukumbu ya kupata taabu msimu uliopita wa Kombe la Shirikisho ilipocheza na Ihefu kwa kushinda kwa penalti.
Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh, amesema kwamba wanatambua ushindani uliopo na namna wanavyopata ugumu kupata matokeo kwa timu za daraja la kwanza ila wapo tayari.
“Timu nyingi ambazo zinashiriki daraja la kwanza ni nzuri na ni ngumu kupata matokeo kutokana na aina ya mbinu walizonazo wakiwa uwanjani pamoja na kutokuwa na cha kupoteza mbele yetu hivyo tunaziheshimu.
“Maandalizi yapo sawa, wachezaji wana morali na walianza maandalizi baada ya droo kuchezwa, hivyo tuna imani ya kupata matokeo yatakayotusaidia kusonga mbele, mashabiki watupe sapoti,” alisema Saleh.
Mashindano ya Kombe la Shirikisho yanaendelea kwa sasa ikiwa ni msimu wa nne ambapo bingwa wa kwanza alikuwa ni Yanga kisha akafuata Simba na anayeshikilia kombe kwa sasa ni Mtibwa Sugar ambaye juzi alitolewa katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment