Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) maarufu kama Kombe la FA, linaendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali huku timu za Ligi Kuu Bara zikieendelea kupukutishwa.
Tayari timu 5 za ligi kuu zimeshatolewa. Timu zilizoondolewa mapema ni Mwadui FC iliyotolewa na Pan Africa kwa mabao 3-1, Ndanda SC iliyotolewa na Transit Camp kwa penalti 3-2 baada ya kutoka suluhu dakika 90, Mbao FC waliotolewa na Dar City kwa penalti 4-2 baada ya kufungana 1-1.
Tanzania Prisons walitolewa na KMC kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kutoka sare ya kutofungana na Ruvu Shooting walitolewa na Mighty Elephant kwa penalti 5-6 baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1.
Timu zilizofuzu ni Dar City, Lipuli FC, Singida United, Transit Camp, Pan African, Kagera Sugar, Friends Rangers, Rhino Rangers, Namungo FC, Reha FC, Majimaji FC, Boma FC, Cosmopolitan, Polisi Tanzania, KMC, La Familia, Coastal Union, Mighty Elephant na Alliance FC.
Mechi nyingine kibao zinaendelea leo ambapo mojawapo ni Yanga itakayokuwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukipiga na Tukuyu Stars.
0 COMMENTS:
Post a Comment