December 9, 2018


Kwa takwimu zilivyo, ni maajabu ya soka pekee yanayoweza kuinusuru Biashara United leo Jumapili kwenye mechi dhidi ya Yanga ndani ya Uwanja wa Taifa.

Biashara itakumbana sura tatu mpya kama sapraizi ambazo mashabiki wa Yanga walizimisi mzigoni ambazo ni Pappy Tshishimbi, Kelvin Yondani na Gadiel Michael zilizokuwa nje kwa matatizo tofauti yakiwemo ya pancha.

Lakini uchunguzi wa Spoti Xtra umegundua kwamba katika wachezaji watatu ambao Yanga inataka kuwasajili kabla dirisha halijafungwa, huenda wakawa jukwaani leo kuwaangalia Biashara.

Timu hiyo ya Mara imeshinda mechi moja tu kati ya 14 zilizopita tena ni dhidi ya Singida United katika Uwanja wa Namfua.

Biashara haijawahi kushinda mechi hata moja hata ikiwa nyumbani mjini Musoma na ndiyo timu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye ligi yenye timu 20.

Timu hiyo imefunga mabao matano tu tangu msimu uanze na leo Jumapili ndio mara ya kwanza inakanyaga kwenye Uwanja wa Taifa ambao Yanga matokeo mabovu waliyowahi kuyapata hapo ni suluhu na Simba ya Bilioni 1.3.

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 38 na haijapoteza mechi yoyote ndani na nje ya Dar es Salaam huku Kocha wao, Mwinyi Zahera akiichukulia mechi ya leo kwa tahadhari kubwa.

Zahera anasema; “Timu zilizoko chini kwenye msimamo wa ligi ni mbaya sana, zinaweza kukubadilikia muda wowote inabidi tuchukue tahadhari kubwa sana kwenye mchezo wetu.”

Kocha wa Biashara, Hitimana Thiery amesisitiza kwamba hawaangalii rekodi zilizopita wanachofanya sasa ni kuanza upya na anaamini wachezaji wake hawatamuangusha.

Hitimana amekiri kuwa na tatizo la ushambuliaji na bado anaangalia uwezekano wa kupata straika japo kwa mkopo kutoka Simba.

CHANZO: SPOTI XTRA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic