January 5, 2019


MSHAMBULIAJI wa Mbao FC ya mkoani Mwanza, Evarigestus Mujwahuki ambaye alifanikiwa kuifungia timu yake bao la ushindi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Alliance uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba leo ataukosa mchezo huo.

Mujahukwi ambaye alifunga bao hilo dakika ya 77 akitokea benchi bado anasumbuliwa na majeraha kwa mujibu wa meneja wa Mbao Almas Mosh.

"Timu yetu inakabiliwa na majeruhi watatu ambao ni Gervas Rambo, Hassan Kasanga na Evarigestus Mujwahuki na tutawakosa katika mchezo huu, ila tuna imani ya kupata matokeo kwa kuwa tuna kikosi kipana," alisema.

Ofisa Habari wa Alliance, James Mwafulango amesema kuwa wanatambua kila timu inahitaji ushindi hivyo watapambana kupata matokeo chanya ili kujiweka nafasi nzuri zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic