January 10, 2019


Baada ya kupata majeraha ambayo yatamfanya aukose mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kiraka wa Simba, Erasto Nyoni amewaambia mashabiki wa timu hiyo wasiwe na presha kwani kwa jeshi lililopo anaamini bado JS Saoura ya Algeria watafungika.

Nyoni ambaye ni mmoja wa mabeki bora ndani ya kikosi cha Simba, alipata majeraha ya goti wakati akiitumikia timu hiyo kwenye michuano ya Mapinduzi Visiwani Zanzibar. Kutokana na majeraha hayo, Nyoni atakaa nje kwa wiki tatu.

Kiraka huyo amesema kuwa licha ya yeye kuumia na kuukosa mchezo huo wa kimataifa lakini hana hofu hata kidogo kwa sababu wachezaji wenzake ambao wamebaki wanaweza kuwamaliza Waarabu.

“Sijisikii vizuri kupata majeraha haya ambayo yananifanya niukose mchezo huu wa kimataifa, lakini hakuna namna kwa sababu tayari imeshatokea na sitakuwepo.

“Lakini niwaambie watu kwamba wasiwe na hofu kutokuwepo kwa kuwa nafahamu wachezaji wenzangu wanaweza kuwachinja Waarabu.

“Kikubwa namuomba Mungu nipone haraka na niwaambie mashabiki wajitokeze uwanjani kwenye mechi yetu hiyo wakawape sapoti ya kutosha wachezaji,” alisema Nyoni ambaye aliwahi kucheza Vital’O ya Burundi.

Simba itacheza mechi yake ya kwanza ya Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi hii.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Nyoni yupo vizuri ni mchezaji mwenye uzoefu anajitambua na ananidhamu ila Juuko Murshidi ni mtu sahihi zaidi katika nafasi ile. Simba au kocha wao wenyewe ndio wanaojipa wakati mgumu usiohitajika katika eneo la beki kwani beki ya wawa,Juuko na Nyoni popote atakapopangwa kwa sababu ni kiraka ingeifanya beki ya Simba kuwa na utulivu zaidi . Kitendo cha Simba kumuweka benchi beki tegemeo wa timu bora ya taifa kama ya Uganda ni kitu cha kushangaza. Juuko huwezi kumfananisha na Pascal wawa Juuko yupo vizuri zaidi. Kama angekuwa raia wa Ivory coast ingekuwa si ajabu hata kidogo kumuona Juuko katika kikosi chao cha timu ya Taifa. Kuelekea mechi na Waalgeria wasiwasi walionao Simba baada ya kuumia Nyoni ni wasiwasi wakujitakia na huwezi kuja kumlaumu Juuko kwa kiwango chochote atakacokuja kukionesha mbele ya warabu hao wa waafrika kwani tayari Simba wao wenyewe ndio waliomtoa mchezoni Juuko kitambo na kumuweka beki huo kisiki katika mazingira ya kutojiamini. Simba walishindwa kumuamini Juuko hata kwenye mapinduzi cup? Na ndio chanzo cha Nyoni kupata majeruhi. Cha kufanya Simba ni kumuandaa Juuko kisaikolojia ya nguvu kabla ya mechi ya kesho ili kumuweka sawa katika game mental fitness .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic