January 6, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amefunguka kuwa kundi lao katika Ligi ya Mabingwa Afrika lipo wazi kutokana na kila timu kuwa nafasi ya kufanya vizuri lakini hofu kubwa ni kikosi chake kukosa uzoefu.

Simba imepangwa Kundi D ikiwa na Klabu ya Al Ahly ya Misri, AS Vita Club yaDR Congo na JS Saoura ya Algeria na itaanza kutupa karata yao Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Aussems ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kundi lao lipo wazi kwa kila timu kuweza kufanya vizuri kutokana na timu watakazocheza nazo lakini anapata wasiwasi juu ya wachezaji wake kukosa uzoefu wa muda mrefu kwenye michuano hiyo kama ilivyo kwa wapinzani wao.

“Binafsi naona kundi letu lipo wazi, linatoa nafasi kwa timu zote kuweza kufanya vizuri kwa sababu ukiangalia AS Vita wamecheza fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita kama ilivyo kwa Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Lakini hofu yangu ipo kwenye upande wa uzoefu kwa kuwa hawa wanacheza karibu kila msimu mashindano hayo tofauti na sisi ambao tuna muda mrefu hatujashiriki, lazima tufanye maandalizi ya kutosha ili tuweze kufanikiwa,” alisema Aussems.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Huu ndio ujinga sasa. Kama tatizo ni uzoefu kwanini wasiongeze wachezaji wenye uzoefu dirisha la usajili na nafasi wanazo!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic