December 18, 2018


Imebainika kuwa uongozi wa klabu ya Yanga haukuachana na straika mpya aliyetajwa kuwa mbadala wa Donald Ngoma, Reuben Bomba kutokana na kufelo mazoezi bali ni kushindwa kufikiana naye dili la kumsajili.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zimeeleza kuwa Yanga walishindwa kuelewana na Bomba ambaye alitokea Congo kuja kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria.

Bomba ambaye alikaa kwa takribani siku tatu za mwanzo alikuja kuteka vichwa vya habari kwa kuelezwa ametmwa na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kumbe sivyo.

Kutokana na kuyumba kwa uchumi ndani ya Yanga imegundulika rasmi kuwa walishindwana kufikiana fedha za kuweza kuingia naye mkataba pamoja na zile za usajili.


4 COMMENTS:

  1. Hivi hawa kina Nyika na wenzake kwa nn wasiwe wakweli.

    ReplyDelete
  2. Ila nyika kwahili la usajili dirisha dogo umechemsha inafaa ujiuzulu uenyekiti wa kamati ya usajili uwezo wako umefika kikomo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic