MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah amechaguliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 2018.
Salah amefanikiwa kuwashinda wachezaji wenzake wawili aliokuwa akishindanishwa nao ambao ni Sadio Mane anayetumikia timu ya Taifa ya Senegal pia anacheza Liverpool na Emerick Aubameyang anayeitumikia timu ya Taifa ya Gabon na klabu ya Arsenal.
Sherehe ya tuzo hizo zilifanyika jana nchini Senegal katika mji wa Dakar, amechaguliwa na viongozi wa Caf, benchi la ufundi pamoja na makocha wakuu ambao ni wanachama 56 wa Caf .
Baada ya kupewa tuzo hiyo Salah alisema kuwa tuzo hiyo ni kubwa kwake, anaipenda kwa sababu alipokuwa mtoto ilikuwa ni ndoto yake kufanikiwa kushinda siku moja.
"Naona fahari kufanikiwa kuitwaa mara ya pili, shukrani zangu nazielekeza kwa familia yangu na wachezaji wenzangu, tuzo hii ni maalumu kwa ajili ya nchi yangu ya Misri," alisema Salah.
Kwa msimu wa mwaka 2018 Salah ameisaidia timu yake ya Livelpool kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa ila hakufanikiwa kumaliza mchezo wake baada ya kuumizwa bega na mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos na walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na kwenye kombe la dunia nchini Urusi hakuweza kufanya vizuri kutokana na kutokuwa fiti kutokana na majeraha.
Mane anachezea Senegal sio egypt/misri
ReplyDelete