December 17, 2018


Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) leo limesema kitendo cha mwanamuziki Diamond Platnumz kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na baraza hilo ni dharau na kubainisha kuwa litatoa tamko kuhusu kitendo hicho.

Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza jana, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba.
Mkali huyo wa Bongo Fleva aliimba wimbo huo jukwaani akiwa pamoja na Rayvanny.

Katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza amesema, “Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi (ya Basata).”

“Basata itakuja na majibu muafaka kwani hapa (Diamond) kaonyesha kiwango cha juu cha dharau kwa baraza, bodi, wizara (Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo) na Serikali kwa ujumla.”

Wimbo huo ulifungiwa Novemba 12, 2018 na baraza hilo kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.

2 COMMENTS:

  1. Kama Kaimbia Mwanza Hana Kosa Na Lazima Maelfu Wa Wana Mwanza Wamshangilie Maana Anaitukuza Mwanza Ya Kimataifa Maana Ukienda Nje Ya Nchi Unapozungumuzia Tanzania Wanajua Dar Pekee So Basata Wawo Wenyewe Ndo Wana Maoni Mabaya Kuhusu Wimbo Huo "Nyegezi Mwanza" Wanataka Tu Kumpiga Pesa Wadhibiti Utandawazi Kwanza Ndo Waufunge Wimbo

    ReplyDelete
  2. Kitaalam...nyimbo nzima ya Mwanza ina maneno machache sana yanaohusiana na eneo husika. Rudi kwenye nyimbo isikilize upya. Hakuna uhalisia wa kichwa tajwa na maudhui yake.
    Kwenye kiswahili tunasema kichwa au jina la nyimbo halishabihiani na maudhui tajwa katika nyimbo.
    Hakuna sifa inayoelekezwa Mwanza wala eneo liitwalo Nyegezi zaidi ya kulitaja kwenye mistar kidogo sana na utajwaji wake umekuwa na ukakasi wa kifani maana si tamathali za semi, istilahi wala kiswahili chenyewe hakina mashiko. Rud kwenye nyimbo niambie wake kwenye nyimbo anapopasia Nyegezi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic