SALEH ALLY APINGANA NA KOCHA YANGA JUU YA YONDANI, AMGUSIA KABWILI
Mwandishi habari za Michezo na Mhariri Mtendaji wa Global Publisher, Saleh Ally 'Jembe' amesema Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amefanya maamuzi ya kukurupuka kumvua unahodha Beki Kelvin Yondani.
Ally amedai kocha Zahera alipaswa kuonana na Yondani kwanza kabla ya kufanya maamuzi hayo kwa kuwa yeye ni mzazi hatakiwa kufanya maamuzi hayo ya kibabe.
Mhariri huyo ameongeza kuwa kwa sasa Zahera ameanza kuibomoa Yanga katika safu ya ulinzi akieleza alianza kumkataa Beno Kakolanya na sasa Yondani.
Ally ameeleza kuwa kwa sasa Yondani hata akirudi Yanga hatajisikia vizuri kutokana na kudhalilishwa hivyo.
Aidha amemtaka kocha huyo kuangalia misimamo yake kabla ya kufanya maamuzi kwani inaweza kuja kumponza yeye mwenyewe.
Ametolea mfano kuwa Mourinho ni kocha mzuri ila misimamo yake huwa inamponza mara kwa mara na ndiyo sababu ilipekea akatimuliwa MANCHESTER UNITED.
Salehe acha tabia za kiswahili, hii ni tabia ya wachezaji wa kitanzania kuchelewa mazoezini, ukiwa kiongozi lazima uwe mfano wa kuigwa ila Kevin tabia yake sio nzuri hata kama anaidai Yanga
ReplyDeleteKwa kweli nashindwa kukuelewa mwandishi nini maana yako juu ya suala hili la Yondani yaani unataka kuwaambia wasomaji wako kwamba Yondani yuko juu zaidi ya timu? au unataka kusema hii ni mara ya kwanza kwa Yondani kufanya hivyo au hasa ni nini nia yako tuweze kukuelewa mara nyengine unaandika vitu vizuri laki kwa hili naona umekosea sana kabla ya kumkosoa Zahera ungekaa kwanza ukajiuliza Yondani amevumiliwa mara ngapi katika suala la kucherewa kurudi? na inakuwaje unaeleza kitu hata miguu hakina iweje suala hilo unalifananisha na la Kakolanya kumbe upeo wako ni mdogo sana wa ufahamu Sheikh Saleh hayo mambo ni mawili tofauti wala hayafanini na kama kweli Zahera ana nia ya kuibomoa Yanga kwa nini anatoa Pesa zake mfukoni kuwapa wachezaji wake? kwa ufahamu wako ni Kocha gani hapa Tanzania aliwahi kufanya hivyo anavyofanya Zahera?
ReplyDeleteHeeheee...hata Kaduguda aliwahi kutoa pesa za kununulia chapati.
DeleteBila nidhamu hakuna maendeleo ya soka. Watanzania tuna tabia ya kujisahaulisha. Ndugu yangu Saleh katika hili umeniangusha sana je umesahau mechi ngapi Kakolanya na Yondani hawakuwepo na timu ilisimama imara? Hii inamaanisha kwamba waandishi na mashabiki wa soka wanashangilia utovu wa nidhamu mchezaji abembelezwe ndipo acheze siku asipojisikia basi hachezi!!! Kisha tunataka matokeo mazuri kutoka timu ya taifa ambayo wachezaji aina hiyo wanategemewa katika hali hiyo!? Vema mkono ukaitwa mkono kuliko kupinda maneno. Kama ulimsikiliza vema Zahera Yanga kupigwa Algeria na Kenya kulikuwa kudhalilika kukubwa kwa timu aliita fedheha na ikiwa magonjwa tutaendelea kuyalea tutarajie fedheha zaidi ba wachezaji wetu kushindwa kujiuza nje wabaki wakicheza ligi yetu pendwa maana hawapaswi kusemwa.
ReplyDeleteZsheara keshajivuruga na keshawavuruga wachezaji wake nanyi mnazidi kumvutuga. Mgema skisifiwa tembo hulijaza maji
ReplyDeleteYondani ajiangalie yukoje na Nadri alikuwaje? Hafanyi kama Nadri alivyokuwa anafanya. Kiongozi unatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kitabia na kiutendaji. Yondani amestahili kuvuliwa unahodha
ReplyDeleteSalehe Unatuvuruga Sisi Mashabiki Wako Kwa Kutuwekea Vitu Vya Kuchonganisha Wanasoka, Mtaalam Ni Mtaalam Tu Kiburi Hakina Nafasi Uwanjani Hasa Kwa Kiongozi Wa Kundi Moja Linalofanya Kazi Ya Kujenga.
ReplyDeleteSaleh wewe ni mnafiki upo kwa ajili ya kuivuruga yanga kupitia kalamu yako....umeacha ishu ya kumpinga manji umehamia kwa zahera endelea kumpa coverage ya kutosha huyo mpinga yanga mwenzio akilimali maana ni wewe tu ndio unayezipa nafasi habari zake za kupinga yanga...ovyo kweli wewe jamaa
ReplyDeleteKwa hiyo yeye kutotoakutotoa taarifa na kuzima Simu haitoshi inabidi tena aitwe asikilizwe na klabu maana yeye ndo mfamle..? Acha kuwapa kichwa wachezajuwachezaji waaina hiyohiyo, amekosea na anastahili adhabu. Alaf kua mchambuzi haina maana ukosoe kila kitu Mzee sometimes pongeza
ReplyDeleteHUWEZI KUMUINGILIA KOCHA KWENYE KUAMUA HATMA YA KAPTENI WA TIMU. KWANI WEWE MWANDISHI ZAHERA ANAKUJA OFISINI KWAKO KUKWAMBIA MEZA IKAE UPANDE WA DIRISHA?
ReplyDeleteAlichofanya zahera nisahihi sana,tunataka makocha wanaodumisha nidham kama zahera,ili kuuendeleza Mpira wetu ambao nimchanga,nandomaana hata timu ya taiga inaboronga wachezaji wetu hawana nidhamu yandani ya kiwanja nanje.yakiwanja.
ReplyDeleteHuu uboza wako utakuponza ushalewa sifa na kujiona wewe kama mungu wa waandishi wote. Huna hekima wala nidhamu ya uandishi, kwanza ulitakiwa udadisi kama mwandishi ungemtafuta kocha akakupa kiini cha yeye kufanya hivyo, labda nikuweke sawa kocha anakaa na wachezaji muda mwingi kuliko wewe unavyodhani unawajua kwahiyo anajua tabia zao kiundani na Zahera ameubeba mzigo mzito sana Yanga, si rahisi kwake kukubali kuharibu CV yake kirahisi kama unavyodhani wewe boza. Zahera ni binadamu na anamapungufu yake, mbona sikukusikia ukisema Omog alikosea kumtoa Mkude unaodha au unaodha alipopewa Boko? Ila kazi yako kuharibu na ndio maana Manara aliwachana live mnapenda kuchochea migogoro, ila wewe na usimba wako kaa nao. USHAURI KWA WANA YANGA BADALA YA KUNUNUA CHAMPION PELEKA HELA ISAIDIE CLUB
ReplyDeleteAlicho kifanya zahera amekosea uwezi ukaanika hali za wachezaji uvyo mbele ya waandishi wa habari mchezaji akicheza chini ya kiwango anawasema itamtokea kama moriny mda sio mrefu
ReplyDelete