OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa uwepo wa mshambuliaji wao tegemeo na nahodha, John Bocco Uwanjani ni dawa tosha kwa wapinzani kutokana na uwezo alionao, na alifanya wapate sare mchezo wao wa watani wa jadi mzunguko wa kwanza.
Bocco alikosekana kwenye mchezo wa Simba na Yanga wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa uliomalizika kwa sare ya kutofungana hali iliyopelekea wapinzani kumwambia Manara kuwa hawakupata presha kubwa kutokana na kutokuwepo kwa Bocco.
"Niliambiwa na beki wa wapinzani kwamba kukosekana kwa Bocco kuliwafanya wacheze bila presha hali iliyosababisha tukashindwa kupata matokeo, hivyo nikiambiwa niwataje washambuliaji hatari hata mara tisa nitamtaja John Bocco," alisema Manara.
Bocco ana mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara aliukosa mchezo dhidi ya Yanga kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata baada ya mwamuzi kutafsiri kitendo cha kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui.
Wapi Boko Simba mmekwisha mheshimiwa Zahera keshatamka kuwa atazowa nyota wote wa Simba kwakuwa anawahitajia. Msimamo wake mkali sana hana masihsra skitsmka hufsnya kweli ns hsrejei nums. Nakulanya chali na Yondani chali sijui kesho nani
ReplyDeleteUwe unasoma Kwanza ulichoandika kabla hujakipost
DeleteZahera akamlipe kwanza kakolanya..Mshahara wa Book pamoja na Kagere ni sasa na mshahara wa Zahera...hawezi chukua hata wa under 21 wa Simba
ReplyDeleteKesha kolewa ba bahati anadhani ndiyo keshachukuwa ubingwa...Ngoja aanze na Azam halafu acheze nje ya Dar zaidi ya nusu ya mechi na atambuwe hata waliokuwa mkiani hawataki kuchuka daraja mzunguko wa pili
ReplyDelete