Kocha msaidizi wa kikosi cha Mbao, Ally Bushiri amefichua siri ya ushindi dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa leo wa hatua ya robo fainali SportPesa Cup uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Bushiri amesema kuwa alitambua kasi na ubora wa kikosi cha Gor Mahia hali iliyomfanya awaambie wachezaji waceze kwa kujiamini bila kuwa na hofu yoyote licha ya kuanza kufungwa bao 1 dakika ya 52.
"Niliwaambia wachezaji wajiamini wanaweza kupata matokeo hali iliyowafanya watafute mbinu mbadala za kupata matokeo na hatimaye tumefanikiwa kushinda ni fahari kwetu na taifa," aisema Bushiri.
Gor Mahia walianza kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Denis Oliech dakika ya 52 baada ya Amos Charles kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Licha ya kuwa nyuma, Mbao waliendelea kupambana na walipata bao la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Abobakar Ngalema akimalizia pasi ya Ally Kombo na kufanya kuwa 1-1.
Matokeo hayo yalidumu mpaka dakika ya 90 ambapo mwamuzi aliamua zipigwe penalti na kuwafanya Mbao kushinda penalti 4-3 zilizofungwa na Said Khamis,Abobakar Ngalema,David Mwasa na nahodha aliyeimaliza Gor Mahia Haroun Shakava huku aliyekosa alikuwa ni Ibrahim Hashimu.
Kwa upande wa Gor Mahia mabao yalifungwa na Francis Kahata, Tusiyenge na Boniface Omond huku Shafiq Batambuze na Haroun Shakava wakikosa kwa upande wa Gor Mahia.
Kwa matokeo hayo Mbao wanafanikiwa kuwavua ubingwa mabingwa watetezi Gor Mahia ambao walitwaa mara mbili mfululizo mwaka 2017 na 2018 na kufanya msimu huu apatikane bingwa mpya.
Mbao inaisubiri Yanga Mwanza
ReplyDelete