UONGOZI wa Simba umesema nguvu ya ushindi kwenye mchezo wa kimataifa watakaocheza Jumamosi itaongezwa na mashabiki hivyo wajitokeze kwa wingi kuwaona mabingwa wakiwa kazini.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema ni wakati wa mashabiki sasa kuipa nguvu timu yao ili ifanikiwe kupata pointi tatu muhimu Uwanja wa Taifa katika mchezo wao dhidi ya JS Saoure ya Algeria.
"Kama kawaida yetu kwa namna ambavyo huwa tunafanya basi ni muda wetu tena kuungana na kufanya kazi moja tu kuwashangilia mabingwa wakiwa kazini siku ya Jumamosi, hakuna namnana nyingine.
Kwa upande wa viingilio, Manara amesema wamepanga kiingilio cha shilingi 5,000 kwa viti vya mzunguko na kawaida itakuwa ni shilingi 10,000.
"Kiingilio kitakuwa ni shilingi 5,000 na 10,000 tu hatutokuwa na VIP na badala yake tutakuwa na Platnumz ambayo ni zaidi ya VIP, hiyo unakuja na gari lako lakini utaliacha pale Serena Hoteli, halafu pale kutakuwa na basi maalum la kwenda uwanjani ambalo litasindikizwa na polisi kwenda na kurudi, huku kukiwa na vitafunwa ndani kwa shilingi laki moja," alisema Manara
Simba wanafikiria kupata mapato zaid badala ya kupata mashabiki wengi wangeshusha kiingilia wangekuwa na mashabiki wengi zaidi hao wanaotaka walipe laki moja wala sio washangiliaji wanaotia hamasa
ReplyDelete