Mtanzania, Abdi Banda anaweza kuendelea kubaki kuichezea klabu yake ya Baroka FC ya Afrika Kusini kwa msimu mwingine, hata kama hapendi.
Hii inatokana na zile taarifa kwamba, uongozi wa Baroka FC umesema hautamuuza kwa kuwa haujapata mbadala sahihi.
Baroka FC imepokea ofa kadhaa, ikiwemo iliyoelezwa kutoka Kaizer Chiefs.
“Bado inaonekena kuna ugumu, lakini kwa sasa siwezi kusema kitu kwa kuwa si msemaji wa klabu kwa sasa,” alisema mmoja wa mameneja wa Baroka FC.
Juhudi za kumpata Banda bado zinaendelea ili aweze kulizungumzia suala hilo.
Kwani baada ya dirisha la usajili kufunguliwa Januari Mosi, Banda alikuwa na matumaini makubwa angeondoka mjini Polokwane na kujiunga na moja ya timu za jiji la Johnnesburg.
Banda amekuwa mmoja wa walinzi tegemeo na aliteuliwa kuwa mmoja wa manahoja wa kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment