January 17, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kikosi chake kipo imara kuwavaa AS Vita na wana uhakika wa kuibuka na ushindi kutokana na maandalizi waliyofanya.

Simba watamenyana na AS Vita ya Congo, Jumamosi ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa wakiwa na kumbukumbu ya kuanza kwa ushindi mbele ya JS Saoura ya Algeria huku wapinzani wao wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi.

Aussems amesema anawatambua wapinzani wake kwa kuwa alipata muda wa kuifuatilia timu hiyo na amegundua ni timu bora haipaswi kubezwa wao wanaifuata kishujaa.

"Tumeanza vizuri ina maana morali ya wachezaji ni kubwa, kazi yetu iliyo mbele yetu ni kuona tunafikia malengo kwa kupata matokeo pia kwenye mchezo wetu wa ugenini bila kuwa na hofu yoyote, hilo linawezekana.

"Kipaumbele kwa wachezaji wangu ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu kwa hali na mali, hali ambayo imenifanya niwape wachezaji mbinu kali zitakazotufanya tupate matokeo, nimewaambia wachezaji nataka mabao ya mapema ili kufanikiwa kuumudu mchezo," alisema Aussems.

Simba wameondoka leo kuwafuata wapinzani wao AS Vita ambao wapo nao kundi D ambalo kwa sasa Simba anaongoza kwa kuwa na idadi ya mabao matatu akifuatiwa na All Ahly ambao wana mabao mawili, As Vita na JS Saoura hazina pointi.

2 COMMENTS:

  1. Hao Al Ahly wenyewe wamepata ushindi wa tabu tena nyumbani kwao na wakicheza na timu yenye wachezaji kumi baada ya beki wa VITA kupewa kadi nyekundu!! Simba wanayo kazi Congo !!

    ReplyDelete
  2. Eti Al Ahyl wenyewe. Nani alikwambia Al Ahyl ndio wenyewe. Simba wana uwezo wa kuwafunga sio AS Vita tu bali hata hao Al Ahyl kwao. Ni kujiamini tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic