January 6, 2019


Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ameweka wazi ukweli kuwa alikuwa akitakiwa na timu moja kubwa nchini Zambia ambayo aliiongoza kwa kipindi kifupi kwa mafanikio bila mkataba, lakini alikataa na kuja Yanga. 

Kwenye kipindi hiki cha Nyundo ya Baruan Muhuza cha Alhamisi hii Januari 3, 2019, Kocha huyo amesimulia safari nzima ilivyokuwa huku akiwataja waliohusika kumshawishi. 

Mbali na hili, kocha huyo amekiri kuwa ndani ya klabu yake ya Yanga kuna matatizo mengi ikiwemo tatizo la pesa, na kusema kuwa amejipanga kumaliza matatizo hayo ndani ya miezi miwili ijayo. 

Zahera pia ameeleza sababu ya ‘kulia’ baada ya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa Desemba 3, 2018 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Zahera amesema waamuzi wa mchezo ule, wachezaji pamoja na mashabiki ndiyo sababu ya yeye kutokwa machozi wakati akiwa kwenye mahojiano na Azam TV.  

Amefafanua kuhusu taarifa za kutumia fedha zake binafsi kuwapa wachezaji huku akiahidi kuyamaliza matatizo yote ya Yanga ndani ya miezi miwili. 

1 COMMENTS:

  1. Kesha lewa ushindi na tuzo za TFF.ushindi wenyewe makocha na wachambuzi wanauita wa bahati. Sio rahisi MTU akataa sehemu yenye neema akaenda pale Hamna mapato ambako wachezaji wanadai mshahara. Ligi bado ilikuwa Simba ichukue Ubingwa mwaka juzi...Siku chache za mwisho rufaa ya kagera ikaharibu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic