January 11, 2019





Duka maarufu la kuuza vifaa vya michezo la Just Fit, limetoa zawadi ya viatu vya kisasa kwa mchezaji mkongwe wa Yanga, Mrisho Ngassa.

Ngassa amekabidhiwa viatu hivyo na bosi wa duka hilo maarufu kama Mzee Karama ambaye alimpa viatu aina ya Adidas.

Mzee Karama amesema wamempa Ngassa ikiwa ni sehemu ya kumuongezea morali.

“Ngassa anaonyesha juhudi tofauti na wengi na sisi tumeona tuna kila sababu ya kumuunga mkono,” alisema.

Duka hilo la Just Fit lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, limekuwa likiwazawadia wanasoka mbalimbali wakiwemo wa Simba, Yanga na timu nyingine.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic