February 2, 2019


MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Ali Kiba amesema watapambana kesho kuibuka na ushindi mbele ya Yanga kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Coastal Union itaingia kwenye mchezo huo ikiwa ina kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuchapwa bao 1-0 lililopachikwa na Makambo.

"tunajua kwamba wao wamejipanga kushinda mchezo wao nasi pia tumejipanga kushinda mchezo wetu hivyo kikubwa ni ushirikiano kwa wachezaji tukiwa ndani ya Uwanja ili tupate matokeo," alisema Kiba.

Coastal Union wamecheza michezo 21 wapo nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic