February 2, 2019


KOCHA wa timu ya Azam FC, Mholanzi pekee ndani ya Ligi Kuu Bara Hans Pluijm ambaye ana uzoefu na michezo ya kimataifa, amesema Simba wananafasi ya kupata matokeo katika mchezo wao wa leo dhidi ya Al Ahly ya Misri endapo watatulia Uwanjani.

Simba leo watakuwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab wenye uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 80,000 ila leo watakuwa 10,000 kutokana na chama cha soka cha Misri (EFA) kutangaza kuwa kimepokea taarifa kutoka mamlaka ya ulinzi nchini humo kuruhusu mashabiki hao.

Pluijm amesema kuwa anatambua uwezo wa wachezaji wa Simba pamoja na aina ya mwalimu waliyenaye hivyo watapata matokeo chanya endapo watajituma uwanjani.

"Mpira ni mchezo wa ajabu ambao hautazami wewe ni nani hasa linapokuja suala la matokeo, ninajua kwamba Simba ni timu bora ndio maana inakutana na timu bora hivyo wachezaji wanatakiwa kutumia akili zaidi uwanjani.

"Kama wamefanikiwa kufika hatua ya makundi kwa nini washindwe kupata matokeo? Basi ni kazi yao sasa wachezaji kuonyesha juhudi uwanjani kila timu inafungika wachezaji wasiwe na hofu," alisema.

Kutoka Championi

2 COMMENTS:

  1. Mholanzi pekee mwenye uzoefu na mechi za kimataifa!!!!Kwani kyba waholanzi wangapi kwenye ligi?
    Makanjanja tabu sana.

    ReplyDelete
  2. Yeye si alifanikiwa kuingia makundi, alishindwaje kushinda!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic