February 23, 2019



KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema anashangazwa na matokeo hasi anayopata hali iliyomfanya aamue kubadili mbinu na kukaa kikao na wachezaji wake ili atafute mbinu mpya zitakazomsaidia kupata ushindi.

Pluijm alianza kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar kisha akapoteza kw Tanzania Prisons kabla ya jana kunyooshwa na mnyama uwanja wa Mkapa, pia alipata sare mbele ya Alliance,Coastal Union na Lipuli.

Pluijm ambaye jana alikubali kupoteza kwa kupata mabao mengi zaidi kuliko ilivyo kawaida yake katika michezo yake yote aliyocheza kwenye ligi ambayo ni 25 na alifungwa mabao 3-1 kwa mara ya kwanza.

Pluijm amesema bado hajajua tatizo la wachezaji wake kwani wanacheza vizuri na wanapambana uwanjani ila wanashindwa kupata matokeo chanya ambayo wanatarajia.

"Kama utasema vijana wangu hawachezi hilo siwezi kukubali ila nadhani kuna kitu ambacho wanakosa kwa sasa, nimeanza kugundua ila kwa kuwa wao ndio wahusika nitakaa nao kisha nizugumze nao kwa ukaribu zaidi," amesema Pluijm.

Licha ya kupoteza mchezo wa jana bado inashika nafasi ya pili ikiwa na poti 50 baada ya kucheza michezo 25 sawa na Yanga ila imezidiwa pointi 11 na vinara hao wa ligi kwani wana pointi 61.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic