February 2, 2019


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeingia vitani na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia baada ya kutoa matamshi ya kuwaonya wajumbe wa mkutano mkuu kuacha tabia za ki Tundu Lissu kwenye kuchafua ama kuleta migogoro kwenye tasnia ya mpira nchini.

CHADEMA kimemtaka Karia kumuomba radhi Lissu ambaye ni wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, bila hivyo wametangaza moja ya mambo watakayofanya ni kuhamasisha wanachama wake kutoshiriki shughuli za TFF.


3 COMMENTS:

  1. Wallace Karia ajitafakari hata Mheshimiwa Rais alisema amepata tumbo kubwa kwa sababu ya madaraka. Anaongoza mpira au siasa. Onyo asiendelee kuingilia mambo ya Chadema. Au TFF ni tawi la chama cha mapinduzi? Na hisi hivyo ndiyo sababu hatutakaa tutoke kwenye mpira. Ligi kuu umeshaharibu kwa asilimia kubwa imekosa mvuto kisa simba!! Pole sana!!!

    ReplyDelete
  2. Utundu Lisu? Usaliti? Licha ya maneno haya kufanana lakini mimi binafsi kama ningekuwa na mamlaka ya kuingiza maneno mapya yenye maana halisi kimatendo kwenye kamusi ya kiswahili basi nigefanya hivyo na neno (utundulisu) lingekuwa neno kamili lenye tafsiri ya usaliti kwa taifa.Nimebahatika kuangalia mahojiano kadhaa anayofanya Tundu Lisu hasa kwenye vyombo vya habari vya nje kwa kweli ni aibu. Ni aibu katika karne hizi kumuona mtu mweusi muafrica akilazimisha wakoloni kuwa kibaraka wao.Ni aibu kumuona Mwafrica kutoka kwenye ardhi ya Julius Kambarage Nyerere akihangaika kuzunguka katika mataifa ya nje hasa yale ya kibepari kulazimisha kuhakikisha Tanzania inakuwa chini ya himaya ya hizo nchi za kikoloni kimaamuzi, na kama vile haitoshi kulazimisha kuja kupangiwa jinsi ya kuendeleza shughuli zao za ndani za kila siku kama taifa huru. Nashangzwa sana na chadema pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kumsapoti Lisu na kumuona shujaa na ule upumbavu anaoendelea kuufanya kwani kamwe hata kwa miaka mia ujinga anaoendelea kuufanya Tundu Lisu haotoleta athari kwa Magufuli,Serikali yake au chama chake bali hapana shaka hata kidogo ujinga huo anaoendelea kuufanya Lisu ni kuchafua taswira ya Tanzania Duniani na athari zake ni kwa watanzania wote hahihalisi upo chma gani. Tundu Lisu ni miongoni mwa watanzania wenye roho mbaya na coward. Hivyo kunusurika kutaka kuuwawa ndio iwe nongwa kutaka kuwaangamizia watanzania wengine nchi yao? Yeye Lisu anajiita msomi bila shaka atakuwa anaifahamu vyema hadithi hai ya akina Kennedy brothers yaani John F Kennedy na Robert F Kennedy wa Marekani. Alitangulia kuuwawa kaka mtu yaani John Kennedy na baada ya kifo chake mdogo wake yaani Robert F Kennedy akaona isiwe shida na kuamua kuendeleza alipoachia kaka yake katika harakati za kisiasa lakini ikaonekana watu wiomdhuru kaka yake nao wakaona isiwe shida kwani walimuua na mdogo wake pia. Lakini baada ya kutokea vifo hivyo vya viongozi wa kisiasa kupitia chama cha Democrat haikuwa mwisho kwa ndugu wa familia ya Kennedy kutumikia siasa za Marekani kwa upendo na uzalendo wa hali ya juu kwani mdogo wao mwengine yaani Teddy Kennedy aliingia kwenye siasa nakuwa mbunge aliekuwa anaheshimika sana kutokana na kuwa mwanasiasa aliesisitiza mshikamano na upendo kwa makundi yote ya siasa bila ya kujali nini kilitokea kwa kaka zake na alijijengea jina yakwamba kama kutakuwa na jambo zito lenye mkingano mzito baiana ya vyama basi Teddy Kennedy alikuwa ni wanasiasa pekee aliekimbiliwa kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo. Hata hii hali ya mashaka ya kisiasa ya sasa Marekani ni baada ya kukosekana watu kama akina Teddy Kennedy. Ukimuona mwanasiasa anakomalia siasa za visasi,watanzania mtu huyo ni wa kuogopwa kama ukoma. Nelson Mandela alikuwa gerezani karibu miaka 30.amekuwa mtu mfu nusu ya maisha yake na mateso ndani yake lakini alippkuja kuachiwa huru hakuwahi kutowa kauli itakayopelekea kuleta maafa zaidi kwa wasauzi Africa wengine. Lisu na chadema kujidanganya yakwamba mataifa ya kigeni yatawasaidia kuingia ikulu kwa kuitoa kafara nchi ni upumbavu wa hovyo na kukosa uzalendo kuliko pindukia. Wapi yaliposhitakiwa mataifa ya ulaya kwa mauaji waliotenda dhidi ya waafrica wakati wa kikoloni? Sio kwamba wakoloni waliua tu waafrica, lakini waliwaua na kukata vichwa vya wahanga wao na kuondoka navyo ulaya na mpaka hivi sasa tunavyozungumza kuna mataifa kadhaa ya Africa Tanzania ikiwa miongoni nwa nchi hizo wamefungua kesi kwenye mahakama za dunia kutaka vichwa hivyo vya waafrica waliouwawa wakati wa ukoloni na kuekwa kwenye majumba ya makumbusho ya mataifa yao kama kumbukumbu na tuzo kutaka kurejeshwa Africa ili mafuvu hayo ya vichwa yaje kuzikwa kwa heshima stahiki kwa tamaduni na mila za kiafrica. Ila kuhangaika anakohangaika Lisu huko nje wazungu wanamuona kama kikatuni na mpumbavu fulani hivi kwani hapana shaka baadhi ya kauli zake za hovyo anazozitoa juu ya kiongozi wake wa juu wa nchi zinawakera hata hao wanaomsikiiliza pengine ndani ya mioyo yao wanasema kwa kauli za kijinga kama hizo basi ulistahiki kutwangwa risasi.

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa inasikitisha kuona Tundu Lisu akihangaika mataifa ya nje kumpiga vita Magufuli kwa tuhuma ambazo nyingi ni za uongo. Hakika lengo la Tundu Lisu na hao wanaomtuma ni kuipaka matope Tanzania na lengo ni moja tu uroho wa madaraka na kwa mataifa ya kigeni kuwa na mtu atakaendana na matakwa yao. Mfano mzuri ni nchi majirani zetu wageni wa mataifa ya nje wanamiliki mpaka mbuga zao binafsi za wanyama. Wageni hao wameushikilia uchumi wa nchi hiyo na rasimali za Tanzania nyingi zikitumika kinyemela katika kukuza vitega uchumi vya wageni hao huku rasilumali hizo za kitanzania zikitumika kwa utambulisho wa taifa jengine bila ya nyaraka maalum na kuikosesha Tanzania mabilion ya shilingi. Kuja kwa Magufuli kumetibuwa kila kitu na kupelekea hali tete kwenye makampuni hayo ya kigeni yaliyojiekesha ubavuni mwa Tanzania kwenye nchi jirani hadi makampuni mengine kufunga shughuli zao kutokana na umakini wa serikali ya Magufuli kusimamia rasilumali ya chi yake isitoroshwe, hivyo kamwe Magufuli hawezi kuwa kipenzi cha makabaila lazima ataundiwa mizengwe na huo ni mwanzo tu makubwa yatakuja ya kumchafua Magufuli ila watanzania waliowengi wanamuelewa Magufuli ni nani .Mfano katika mahojiano ya Lisu na mtangazaji wa BBC idhaa ya kizungu. Lisu anazua uongo kwa kusema kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa ikiuwa wananchi wake kule kibiti na kuwatosa baharini lakini ukweli ni kwamba serikali ndio iliokwenda kuzuia mauaji ya wananchi wasiokuwq na hatia kule kibiti na kupelekea hata askari kadhaa kuuwawa katika mapambano kuhakikisha hali ya amani inarudi kibiti. Hivyo leo utakuja kunambia mauaji ya watoto kule Mkoani Njombe serikali ina mkono wake? Sasa kwa kweli ukimuona mtu kwa makusudi akipotesha uhalisia wa mambo yaliyotokea hapa nchini kwa mataifa ya kigeni na kuipaka nchi taswira chair nchi duniani hukaa nikajiuliza kama kweli huyu Lisu ni mzima wa akili au kachanganyikiwa au anahangaika kujenga kesi ya ukimbizi ili apatiwe hifadhi ya kuishi ulaya maisha yake yote kwa kisingizio cha kuhofia usalama wake kama akirudi Tanzania ila lazima atakuwa na kesi ya kujibu siku atakayotua Tanzania kama atarudi kwakuzungumza uongo juu ya serikali..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic