February 3, 2019


Kikosi cha Simba kimekubali kufungwa mabao 10 katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Idadi hiyo ya mabao imekuja kufuatia kupokea kichapo kingine cha mabao 5-0 kutoka kwa miamba wa Afrika, Al Ahly ya Misri jana usiku.

Kipigo kimekuja kwa Simba ikiwa ni baada ya kutandikwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita ya Congo kwenye mchezo ambao ni wa kundi D.



Msimamo hivi sasa unaonesha Simba imeshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 3 pekee huku Al Ahly wakiwa kileleni na pointi 7.

Katika nafasi ya pili AS Vita ambao jana walienda sare na JS Saoura wamefikisha alama 4.

11 COMMENTS:

  1. Kweli sio matarajio ya wengi kuiona Simba ikifungwa hivyo namna hii unaweza kuita aibu ukipenda ila Jumamosi hiyo hiyo TP Mazembe kampiga mtu goli nane mtungi 8-0.kufungwa kwenye mashindano ni kitu cha kawaida ila kinachokera kwenye hii simba ya sasa ni ile hali ya baadhi ya viongozi wake kushindwa kuwajibika ipasavyo na mbaya zaidi ni ile hali inayoonesha viongozi hao kutojali maoni ya watu wengine. Simba kweli ipo kwenye kipindi cha uimarishaji wa timu kuanzia timu yenyewe hadi miundo mbinu lakini Simba ni timu kongwe na brand kubwa. Js Saoura hata wangefungwa kumi bila kwenye mechi zao wanaweza kujitetea na ukawafahamu ni timu iliyoanzishwa 2008. Simba sio timu ya kuzalilishwa hivyo namna hii. Ni timu ya kuwa na mikakati imara ya kivitendo sio blah blah. Ligi yetu duni sawa lakini simba haohao wanashindwa kufanya vizuri kwa timu kama mashujaa au Mbao hapo kama viongozi wa Simba vichwa vyao vinafanya kazi kweli lazima wangetambua yakuwa timu yao ina matatizo tena makubwa.
    Simba haiwezi kitaabika kuifunga mbao alafu wajidanganye wana uwezo wa kuifunga El ahly. Kocha wa Nkana alitoa ushauri wa bure kabisa yakwamba Simba mnaingia hatua ya makundi lakini mpigane piga ua muimarishe beki yenu. Wadau kadhaa walitoa ushauri huo huo lakini hakuna lilofanyika kurekebisha kasoro. Js Saoura kafungwa 3-0 na Simba kilichofuata ni kocha kitimuliwa.Simba kafungwa tano Mtungi 5-0 na As vita lakini hakuna chochote pale simba cha vitendo cha maana kilichofanyika cha marekerebisho kwenye timu isipokuwa blah blah. Simba kuna tatizo kama si matatizo kwenye timu. Kama si kocha wachezaji na kama si wachezaji viongozi lakini lazima uozo utakuwa upo pahala na ile azma ya Mo kuifanya simba kuwa timu shindani barani Africa hakutarajia timu ingeanza na aibu ya aina hii.

    ReplyDelete
  2. Acha upuuzi Yanga mwaka Jana kombe LA shirikisho walipigwa 4 Algeria, wakapigwa 3 Nairobi na 2 Kigali...ukiacha walizofungwa Dar!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga tunazungumzia5-0❎ 2

      Delete
    2. Hi ujinga kulinganisha GOr Mahia, Rayon Sport na timu kama All ahly au AS Vita...Yani hapo no ubongo maji...Hizo timu zote za Afrika mashariki zilimlamba Yanga.

      Delete
  3. Nimependa maoni ya mtu wa kwanza. Anajua kuchambua mpira na sio mradi kuandika tu kama huyu vhizi wa pili. Simba tunahitaji marekebisho na kupata wachezaji wa kweli kwenye kiungo na ulinzi. Kocha nae hafai. Anampangaje dogo wa simba B (Rashid Juma) dakika 90 kwa mechi nzito kama ile? Dogo alikuwa hakabi na hajui kinachoendelea maana mechi ilikuwa kubwa sana kwake. Ajabu kocha anamtoa mtu mzoefu (Kagere) na kumwacha Rashid akitegemea Rashid angeleta mabadiliko. Huyo kocha ni bomu. Alipaswa kutoa kinda na kuingiza mzoefu na mwenye uwezo

    ReplyDelete
  4. Huu si muda wakulaumiana mpira umekwisha tujipange tulipo teleza, tunaamini hakuna anaye penda kufungwa ama kushindwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hapana aisee...kocha awajibike hakuja kutengeneza CV yake Simba kwa kupigwa 10-0.Bora hata Julio apewe timu

      Delete
  5. Kabisa kocha anaweza kuwa mzuri lakini umeona wapi timu inayoshiriki mashindano makubwa kama ya club bingwa barani kocha wake hana saidizi?

    ReplyDelete
  6. Hayo ndio matokeo ya kuwa na ligi mbovu tunashindwa tukienda kushiriki mashindano ya kimataifa

    ReplyDelete
  7. Tatizo in Dana potufu tilionayo mashabiki wa Bongo, Simba akimfunga Ndanda basi eti ni timu nzuri, Yanga anashinda kwa bahati bahati eti ni timu nzuri...Sumba na Yanga hakuna timu hapo. Tuache ushabiki usio na maana. Sumba amestahili hizo goli tano, hata Yanga angeenda angekula hizo tano.

    ReplyDelete
  8. Kocha apigwe chini kwanza ndipo kikosi kisukwe upya. Kwa mtindo huu tutafungwa hata hivi viporo vyetu vya ligi ya bongo. Kocha hana mfumo mbadala baada ya kufeli ule wa awali. Na mbaya zaidi makocha wa timu nyingi wameshamsoma mbinu yake hiyo moja, hivyo wanamtageti wakijua hawezi kutoka. Huyu kocha atatukosesha kila taji msimu huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic