February 25, 2019



ZILE tambo za mwanzo kwamba kinachopona machinjioni ni kisu tu zimetimia baada ya kisu kuonekana mitaa ya Jangwani iliyo chini ya utawala wa kocha mkuu Mwinyi Zahera na kuwafanya wana Namungo kukubali matokeo.


Dakika 83 zilitosha kuonesha makali ya kisu cha wana Jangwani kwenye uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi baada ya Deus Kaseke kumimina krosi maridadi iliyomkuta Heritier Makambo katika eneo sahihi na kumalizia kichwa kilichozama wavuni.

Mlinda mlango wa Namungo FC ambaye dakika zote 83 alikuwa nyota wa mchezo aliishiwa nguvu baada ya kushtuka mpira upo kambani, licha ya jitihada za Namungo kutafuta sare walikuwa wamechelewa kwani safu ya ulizi ya Yanga haikuruhusu kuchinjwa ugenini.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga isonge mbele hatua ya nane bora ikisubiri mpinzani wake ambaye watakutana naye baada ya droo kuchezwa hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic