February 24, 2019


MKURUGENZI  Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo usiku wa jana alikuwa miongoni mwa waliokabidhi tuzo  za Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, (SZIFF 2019).

Tuzo hizo zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Februari 23,2019 ambapo Shigongo alitoa tuzo katika Kipengele cha Muigizaji Bora wa Kike katika World Cinema ambapo walitangazwa washindi  wawili, Leena Alam kutoka Afghanstan na Myra Vishwakarma kutoka India.

Hii ni mara ya kwanza kwa Shigongo kufanya hivyo hali inayomfanya aweke historia hizo za tuzo ambazo zilihudhuriwa na watu mashuri na wanasiasia kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic