February 25, 2019



HIZI hapa zimefanikiwa kupenya hatua ya 16 bora kwenye kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali:-

Singida United kutoka mkoani Singida iliifungashia virago Coastal Union ya Tanga kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Chamazi.

Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime iliifungashia virago timu ya Boma kwa kuifunga mabao 2-1.

KMC ya Dar es Saalaam iliwaondoa mabingwa watetezi Mtibwa Sugar baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ilishinda kwa penalti 4-3 Uwanja wa Chamazi.

Lipuli ya matola ilishinda dhidi ya Dodoma ya Julio kwa mabao2-1.

Yanga  imeichinja Namungo FC kwa bao 1 la usiku Uwanja wa Majaliwa.

Alliance FC ya Mwanza imeitungua Dar City ya Tanga mabao 3-0.

African Lyon ya Dar imeitungua Mbeya City ya Mbeya kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya mabao 2-2 Uwanja wa Uhuru,

 Bingwa wa msimu huu atakuwa ni mpya kutokana na kuondoshwa kwa bingwa mtetezi Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic