February 25, 2019


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, mwenye mabao 12, ametumia dakika 540 kufunga bao lake la 12 ikiwa ni baada ya kucheza mechi tano mfululizo bila kutupia na ya sita akafunga.

Mara ya mwisho Makambo alifunga dhidi ya Mbeya City ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku yeye akifunga bao la ushindi kwa kichwa na kuisaidia timu yake kubeba pointi tatu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Baada ya hapo, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko na Makambo akarejea kwao DR Congo ambapo alichelewa kurejea Bongo kutokana na matatizo ya kifamilia, akarejea baada ya mchezo wa Yanga na Mwadui ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Makambo alicheza michezo sita iliyofuata ambayo ilikuwa dhidi ya Stand United na Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, kisha sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union, akacheza dhidi ya Singida United na kulazimishwa suluhu, pia kwenye mchezo wa nne ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania ambayo Yanga ilishinda 1-0.

Mchezo wake wa tano dhidi ya Simba, Yanga ilifungwa 1-0, kabla ya Makambo kuibuka kwenye mchezo wa sita dhidi ya Mbao ambao Yanga ilishinda 2-1 kwa mabao ya Makambo na Amissi Tambwe.

Mechi hizo sita ni sawa na dakika 540 kupita Makambo ndipo akafunga tena kwa kichwa bao lake ambalo linamfanya afikishe mabao 12 msimu huu akiwa kileleni kwa ufungaji sawa na Salim Aiyee wa Mwadui.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic