February 23, 2019


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa mkoani Lindi kwa kibarua maalum dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la FA kesho Jumapili, Kocha Mwinyi Zahera amewataka wachezaji ambao mikataba yao inaelekea kuisha wajitume vilivyo.

Zahera ameeleza kuwa kwasasa anachoangalia zaidi ni kuona kila mchezaji anapambana vya kutosha ili kujiwekea nafasi ya kusalia katika kikosi cha Yanga msimu ujao.

Kocha huyo amewataja wachezaji Papy Tshishimbi, Klaus Kindoki, Thaban Kamusoko na Amis Tambwe kuwa mikataba yao inaelekea kumalizika baada ya msimu huu.

Kutokana na mikataba yao kuelekea ukingoni, Kocha huyo ametoa angalizo kwa kuwataka wapambane na wamshawishi ili azungumze na mabosi wake waongezewe mikataba endapo watafanya vizuri.

Tayari taarifa za ndani zinasema mabosi wa Yanga wako kwenye harakati za kuanza kuboresha mikataba ya wachezaji baadhi ambao wanaona wataisaidia timu.

Ukiachana na waliotajwa na Zahera, straika Ibrahim Ajibu naye anatajwa kuanza kufanyiwa mchakato wa kumwaga wino mwingine ndani ya kikosi cha Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Mbona Ajibu, Yondani na wengi wengine hawamo nao wanajulikana kuwa mikataba yao imeshafika ulingoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic