February 23, 2019


BILA kupepesa macho, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amemtaja kiungo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa ndiye injini kwenye kikosi chake.

Fei Toto amekuwa kati ya wachezaji tegemeo kwenye idara ya kiungo ya Yanga, ambapo amekuwa akitumika mara nyingi kama kiungo mkabaji.

Zahera alisema kuwa, Fei Toto ni mchezaji mwenye akili kubwa ya kuweza kushika vitu kwa haraka wakiwa mazoezini na kisha vitu hivyo huwa anavifanya akiwa kwenye mechi.

Na mara nyingi vitu afanyavyo vimekuwa na faida kwa timu, huku akitolea mfano wa vitu kama pasi, chenga na mabao ya mbali ambayo huwa anafunga.

“Fei toto ni mchezaji ambaye ana akili kubwa sana ya kushika vitu na kuvifanyia kazi bila kujali utakuwa umepita muda gani. 

“Utakuta akipiga chenga mazoezini, jua kwenye mechi atafanya hivyo hivyo na hata yale mabao yake huwa anafunga kwanza mazoezini na akija kwenye mechi hufunga kwa mtindo ule ule,” alisema Zahera.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic