February 25, 2019


Kocha wa klabu ya Singida United Dragan Popadic, amesimaishwa michezo mitatu baada ya kumzonga Mwamuzi wakati akitekeleza majukumu yake uwanjani.

Popadic aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ndanda FC.

Kutokana na tukio hilo, Kamati ya Nidhamu ya TFF ilikaa na kujadili kisha kuja na maamuzi ya kumsimamisha jumla ya mechi hizo tatu.

Katika mchezo huo Ndanda FC ilifanikiwa kuitandika Singida jumla ya mabao 2-0, mechi ikipigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.


3 COMMENTS:

  1. Hii kamati mbona ikihusu kesi ya timu mojawapo nä wachezaji wake inakuwa haina muda wa kukutana lakini kama ni:timu nyingine adhabu zinatolewa haraka sana.
    Ni scandal mchezaji kumpiga mwenzake kiwiko na
    bado anaendelea kucheza kama hamna kilichotokea. Justine delayed is justice denied.
    Halafu kocha na wanachama nä wapenzi kazi kulalama eti kuna njama dhidi yao.
    Give me a break.

    ReplyDelete
  2. Unajua hii ni Tanzania na wanaotuongoza ni watanzania,na kama unavyojua watanzania tuna giza yani hata tupate elimu bado giza litatusumbua tu kwani elimu yako itakua mfano wa tochi sasa ukumbuke upo kwenye riadha alafu ni usiku je ile tochi itaweza kukusaidia kweli?jibu ni hapana,basi ahsanteni.

    ReplyDelete
  3. Unajua hii ni Tanzania na wanaotuongoza ni watanzania,na kama unavyojua watanzania tuna giza yani hata tupate elimu bado giza litatusumbua tu kwani elimu yako itakua mfano wa tochi sasa ukumbuke upo kwenye riadha alafu ni usiku je ile tochi itaweza kukusaidia kweli?jibu ni hapana,basi ahsanteni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic