February 2, 2019


ALIYEWAHI kuwa kipa wa Yanga, Manyika Peter amefunguka kuwa, kipa Beno Kakolanya alistahili kumuomba msamaha kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo na kudai kuwa watu wanaomzunguka si sahihi.

Beno aliingia katika mvutano na Zahera ambaye naye aliamua ‘kumfungia vioo’ katika kikosi chake kufuatia kugomea baadhi ya mechi kutokana na madai ya kudai haki zake, jambo ambalo lilimkasirisha kocha huyo, hivyo kufikia uamuzi wa kuomba kukatisha mkataba wake.

Manyika alisema kuwa watu wanaomzunguka Beno si shahihi kwa kuwa wanamshauri vibaya mchezaji huyo kwa kuwa alitakiwa kuomba radhi.

“Kuamua kuomba kukatisha mkataba na klabu hiyo ni maamuzi yake mwenyewe, lakini kwa jinsi inavyoonekana watu wanaomzunguka si sahihi kwani wanaonekana kumshauri vibaya.

“Kitendo anachokifanya hakina afya katika maslahi ya kazi yake kutokana na kutokuwa na nidhamu kwani mchezaji sahihi hawezi kufanya kitu bila ya kuwa na nidhamu.

“Ukiwa siyo mtu mwenye nidhamu basi unaweza kufanya vitu ambavyo siyo sahihi, angekuwa na nidhamu angemuomba radhi mwalimu ili aendelee kucheza, yeye anaomba kuvunja mkataba, mpira una mambo mengi.

“Huko anapotaka kwenda akimkuta mwalimu kama huyo ama Zahera akapata nafasi ya kufundisha timu ambayo yeye atakwenda, kwa hiyo ataondoka au!

“Watu alionao hawamshauri vizuri na ikiendelea hivi safari yake ya mpira itakuwa fupi kwani mpira ni nidhamu,” alisema Manyika.

2 COMMENTS:

  1. mtotot wako mwenyewe tena kipa kama Kakolanya baada ya Singida united kutomlipa ulimshauri avunje mkataba na hakuna mtu aliyesema kashauriwa vibaya leo Kakolanya anadai haki yake unamwambia kazungukwa na watu wabaya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic