February 2, 2019


Mashabiki wa Timu ya Simba wamejipa matumaini kuwa kikosi chao kitaibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo Jumamosi saa 4 Usiku kwa saa za Kitanzania kati ya Simba na wenyeji Al Ahly ya Misri.

Wakizungumza na Global TV Mashabiki hao wamesema kuwa timu yao imefanya maandalizi japokuwa timu ya Al Ahly ipo vizuri Zaidi katika mpira lakini pia mpira ni dakika tisini wamejindaa kwa matokeo yoyote japokuwa asilimia kubwa wanaipa timu yao.

Kwa upande wake shabiki wa Yanga amesema kuwa mechi hiyo itakua ngumu kwa Simba kutokana na utofauti wa Timu za Tanzania na Misri.

Simba katika mchezo uliopita walifungwa mabao 5-0 na AS Vital ,ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, leo watacheza mechi ya tatu na Al Ahly kwenye Uwanja wa Borg El Arab.

Simba sasa wapo nafasi ya tatu kwenye kundi lao wakiwa na pointi tatu wakati Ahl Ahly ni vinara wakiwa na alama nne, AS Vita ya pili na pointi zao tatu huku JS Saoura wakiwa mkiani na alama yao moja.

2 COMMENTS:

  1. Mashabiki wa simba wajiandae na aina yoyote ya matokeo katika mchezo huo kwani kiukweli kuwafunga Ahly kwao sio kitu rahisi hata zile habari za kusema sijui Ahly wanamajeruhi wengi ni moja kati ya mbinu kubwa kabisa a warabu kuwapumbaza wapizani wao si ajabu kuja kuwaona baadhi ya majeruhi wamo wenye listi ya mchezo wa leo . Kwa kiasi fulani jukumu lipo kwa wachezaji wa Simba zaidi kujituma kwa pamoja ila mtu yeyote mwenye akili yake timamu lazima anakuwa na tahadhari anapokuwa ugenini hawezi kujiachia tu kama yupo nyumbani. Na simba wanatakiwa kuwa na tadhari kubwa katika mchezo wa leo hasa katika dakika za mwanzo za mchezo. Mfaransa wa Simba kocha alietimuliwa kabla ya huyu alituonyesha watanzania vipi unatakiwa kujipanga unapocheza ugenini vitu vingine wachezaji wenyewe wanatakiwa kuwa na maamuzi ya mechi badala ya kusubiri kocha kuwaelekeza nini cha kufanya.

    ReplyDelete
  2. Tanzania bado tuko nyuma sana. Hata timu za kenya hatuziwezi. Simba isitegemee hata droo. Katika mechi za hapa nyumbani simba haiko viziri na wakifungwa wana sababu moja tuu tuko kwenye maandalizi ya kombe ya Afrika. Matokeo na ukweli ni 5 waluzofungwa na timu ya Kongo. Fomasheni ya kocha ni mbovu sana pasi nyingi kati kati inasababisha timu pinzani kurudi haraka golini kulinda.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic