February 23, 2019


Kikosi cha timu ya Namungo kesho Jumapili kitawakosa wachezaji wake wanne katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Yanga utakaopigwa huko Lindi.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi, Bakali Malima 'Jembe Ulaya' amesema wachezaji hao wanasumbuliwa na majeruhi.

Ulaya amewataja wachezaji hao kuwa ni Mbaraka Yusuph anayesumbuliwa na maumivu ya goti sambamba na Jamal Machelengwa aliye na majeraha ya enka.

Ukiachana na wawili hao, kipa Steve John naye atawakosa Yanga akisumbuliwa na Maralia pia Mustapha Makacho anayeumwa na goti.

Yanga inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mechi iliyopita dhidi ya Mbao FC katika Ligi Kuu Bara na salaam zimeshatumwa Mbao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic