ACHANA KABISA NA SAOURA, KOCHA SIMBA AWATAJA WANAOMUUMIZA KICHWA ZAIDI
KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa hawazi kupata ushindi katika mechi yake na JS Saoura bali anaumiza kichwa jinsi ya kuifunga AS Vita inayonolewa na Florent Ibenge ambaye ni swahiba mkubwa wa Mwinyi Zahera wa Yanga.
Simba ambayo iko nafasi ya pili katika kundi D, ikiwa na pointi sita, nyuma ya vinara wa kundi hilo, Al Ahly ya Misri wenye pointi saba wakat JS Saoura kutoka Algeria ikiwa na pointi tano huku As Vita ya DR Congo ikiwa na pointi nne.
Simba inaondoka Dar es Salaam leo Jumanne ambapo Jumamosi itacheza na JS Saoura ugeninikabla ya kuvaa na AS Vita Machi 16.
Akizungumza, Aussems alisema; “Nilisema mapema hili kundi lipo wazi sasa na kila mmoja anaona hali halisi sasa tupo wapi na tunayo nafasi kubwa ya kwenda robo fainali kama tutafanikiwa kuifunga AS Vita hapa kwetu.”
“Na ndiyo jambo kubwa ninalolipa nafasi kubwa kwenye akili yangu kuelekea kwenye mchezo huo.
“Matumaini yangu yapo kwenye mechi na As Vita siyo wale JS Saura labda pengine itokee sare lakini sioni dalili za kuweza kufanya hivyo kwa sababu soka la Afrika limekuwa na mambo mengi hasa kwa upande wa timu mwenyeji ndiyo maana najipanga na As Vita kufanya kile ambacho tuliweza kufanya kwa Nkana,” alisema Aussems.
Huyu kocha nae tabia yake ya kuondoa moyo wa kupambana ugenini kwenye mechi za klabu bingwa Africa ndio chanzo kikubwa cha Simba kupokea vipigo vya aibu. Kocha gani anaewatamkia wachezaji wake kuwa mechi hii hatuwezi kushinda? Wachezaji wa Simba wana uwezo wa kushinda hata katika mechi za ugenini Africa ila kocha wao hajiamini. Wachezaji walewale wa Simba walioifunga Saoura iliokwenda kuvuna points kwa As vita ilioipiga Simba kipigo cha aibu Kinshasa inaonesha yakwamba Simba haipo vizuri kwenye benchi la ufundi kuwaandaa wachezaji wao kukabiliana na mechi za ugenini Africa. Wachezaji walewale walioifunga Ahly Dareslaam ndio waliopokea kipigo cha aibu ugenini na hao hao Ahly kule Misri hii inaonesha dhahiri wachezaji wa Simba wana uwezo kimpira ila tatizo lipo kwenye benchi lao la ufundi linapokuja suala la mechi za ugenini Africa. Sasa viongozi wa Simba lazima ifike mahali wajisemee enough is enough yaani imetosha sasa kwenda kupata aibu na machungu ugenini yasifanana na hadhi ya timu lazima wamkomalie kocha wao kwenye hii mechi na Js Saoura iwe na matokeo tofauti na yale ya Kogo na Misri na hasa ukitilia maanani yakwamba hata mechi ya As vita na Simba Dareslaam haitakuwa rahisi hivyo. Kwa wachezaji wa Simba hasa wazawa bado hawaja yatumia mashindano hayo ya Africa kwa faida na mechi hizi za ugenini nchi kama Algeria ndio mechi zenye macho ya wengi zaidi wenye kutafuta wachezaji kwa maslahi mapana zaidi. Kwa hivyo mchezaji lazima wazikamie hizi mechi kufanya makubwa kuisaidia timu na ili waonekane na vilabu venye maslahi zaidi na hata kama itatokea timu imeshindwa kupata ushindi lakini jitihada lazima zionekane yasijirejee tena yale ya Kinshasa na Alexandria kule Misri. Binafisi nilitarajia kumuona kocha wa Simba kuelekea kwenye mechi hii na Saoura akiwatangazia wachezaji wake kuwa mechi hii na Saoura ni fainali piga ua lazima washinde kwani kunako jitihada hakuna lisilowezekana lakini kusema ukweli kauli zake za kusema hatarajii timu yake kupata ushindi Algeira zinatia kichefuchefu na hakika zinawavunja moyo wachezaji pia.
ReplyDeletekama huna imani ya ushindi unaondoka mapema kwenda kufanya nini? au ndo mambo ya mind game ili ukawashangaze huko waamini tumekata tamaa ili walegeze makamuzi?
ReplyDelete