March 25, 2019


KIKOSI cha Simba kinaanza mazoezi leo Jumatatu kujiwinda dhidi ya Mbao FC baada ya kupewa mapumziko mafupi na uongozi wa klabu hiyo.

Simba walipewa mapumziko mara baada ya mchezo wao dhidi ya AS Vita ambao ulipigwa Jumamosi iliyopita na timu hiyo kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupangwa na TP Mazembe ya Congo ambayo watavaana Aprili 5, mwaka huu.

Simba itarejea kwa mara nyingine katika ligi kuu Jumapili ijayo itavaana na Mbao FC katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo ndipo timu hiyo imehamia baada ya Uwanja wa Taifa kufungwa kwa muda.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kikosi chao kitaanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mbao.

“Wachezaji wataanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu tuliwapa mapumziko baada ya mechi na AS Vita Club na baadhi walikwenda kwenye majukumu yao ya timu ya taifa hivyo wataanza kurejea.

“Wataanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu na Mbao FC ambao tunaenda kucheza Morogoro na uwanja ule unaendelea kurekebishwa kwa sasa ili kila kitu kiweze kwenda sawa sababu tunakwenda kuutumia,”alisema Meneja.

Simba imehamishia makazi yake katika Uwanja wa Jamhuri na mchezo wa awali ambao walikutana na Mbao katika Uwanja wa CCM Kirumba Simba ilipoteza kwa bao 1-0.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic