KISA WAKONGO, SIMBA WAIVAA TFF
UONGOZI wa Simba umepeleka maombi maalum kwa Bodi ya Ligi inayofanya kazi kwa karibu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania kupangiwa tarehe nyingine.
Simba itatakiwa kucheza dhidi ya wapinzani wao hao katika mechi ya Ligi Kuu Bara mnamo Aprili 3, mwaka huu, kisha Aprili 6 inatarajiwa kuwa na kibarua mbele ya TP Mazembe katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Robo Fainali.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema kwa sasa wanasubiri majibu tu ambayo watayapata kutoka TFF baada ya kupeleka maombi yao.
“Tumepeleka maombi yetu kwa TFF kuona namna gani tunaweza kufanya ili tupate muda wa kujiandaa kwa mechi yetu ya kimataifa dhidi ya Mazembe, tunataka mechi dhidi ya JKT Tanzania isogezwe mbele.
“Barua ilishakwenda, kwa hiyo sasa hivi tunasubiri majibu yao tuone yako vipi wakati tukiendelea kujiandaa na mechi yetu na Mbao FC,” alisema Rweyemamu.








Sababu ya msingi ipo na TFF maombi hayo wayatie maanani na kuyapa jicho la huruma na ndio iweze kuiletea fahari Tanzania
ReplyDeleteVitu vya kushangaza sana. ukisikia mtu anajipiga risasi mwenyewe ya mguu kumrahisishia kazi adui basi ni hii ratiba ya bodi ya ligi kwa Simba. Yaani ni kama hujuma kwa Simba lakini ni hujuma kwa taifa pia wahusika wanatakiwa kuwa makini kwani hatua walipofikia Simba ni hatua ngumu zaidi na hasa timu unayocheza nayo yaani tp mazembe. Unaitaka Simba ikafanye vizuri mbele ya tp mazembe bila yakuwa na muda wa kuindaa timu maana yake ni nini? Hasa ukichukulia kuwa Simba sasa inabidi isafiri kwenda na kurudi kutoka Morogoro.
ReplyDeleteSiku zinatosha... Kama hamtaki kucheza ligi jitoeni.... Ila msijenge mazingira ya kubebwa baadae mje mpange matokeo
ReplyDeleteSiku zinatosha... Kama hamtaki kucheza ligi jitoeni.... Ila msijenge mazingira ya kubebwa baadae mje mpange matokeo
ReplyDelete