March 24, 2019


Straika wa Simba, Meddie Kagere amemjibu Zahera kwamba asitarajie wapoteze kwani wanajua hesabu zote zilivyo.

“Kitu pekee ambacho kitatupa fursa ya kuwa vinara ni ushindi hakuna jambo jingine ambalo tunatakiwa kufanya kwa sasa kwenye ligi.

"Wapinzani wetu walipata matokeo na ndio maana wako pale walipo nasi njia yetu ni moja kushinda.

“Ushindani ni mkubwa na mara zote tumekuwa tukipambana na tunashukuru tunapata matokeo.

"Kikubwa ni kutokata tamaa na mashabiki waendelee kutupa sapoti kuwa vinara ni suala la wakati tu,” alisema Kagere. 

Mpaka sasa Kagere ametupia mabao 13 kwa sasa akimuacha Heritier Makambo wa Yanga mwenye mabao 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic